Elimu mbadala, ambayo pia hujulikana kama elimu isiyo rasmi, ni dhana yenye maana pana na inayoweza kutumiwa kurejelea aina zote za elimu zilizo nje ya elimu ya kawaida (kwa watu wote na viwango vyote vya elimu).

Hujumuisha si tu mitindo ya elimu inayokusudiwa wanafunzi wenye mahitaji ya pekee lakini pia mitindo inayolenga hadhira ya jumla na kutumia mitindo na falsafa badala ya elimu.

Elimu mbadala mara nyingi huwa matokeo ya mabadiliko katika elimu yaliyotokea katika misingi mbalimbali ya falsafa ambayo kwa kawaida ni tofauti na elimu ya jadi ya lazima. Mabadiliko mengine yana misingi ya kisasa, kiutafiti au kifalsafa, ilhali mengine ni miungano isiyo rasmi kati ya walimu na wanafunzi wasioridhika na masuala fulani ya elimu hiyo ya jadi.

Elimu mbadala hii ambayo ni pamoja na shule za tabia, shule badala, shule zinazojitegemea na masomo ya nyumbani hutofautiana pakubwa, lakini zote hutilia maanani umuhimu wa idadi ndogo ya wanafunzi darasani na mahusiano ya karibu kati ya wanafunzi na walimu. Vilevile husababisha hali ya umoja.