Elvis Kamsoba
Elvis Kamsoba (alizaliwa 27 Juni 1996) ni mchezaji wa soka wa Burundi ambaye anacheza kama mshambuliaji wa klabu ya Melbourne na timu ya taifa ya Burundi.
Kazi ya klabu
haririMelbourne Victory
haririKamsoba alisainikatika klabu hiyo ya Victory iiliyopo katika A-League kwa mkataba wa miezi 18 mnamo 3 Januari 2019. Alicheza mechi yake ya kwanza katika klabu ya Melbourne mnamo 9 Januari 2019 kwenye mechi ya A-League dhidi ya klabu ya Adelaide United. [6]
Kazi ya kimataifa
haririMnamo 24 Machi 2019 alithibitisha kwamba alikuwa amekataa wito wa kwenda katika timu ya taifa ya Burundi kwa sababu Elvis alikuwa na uraia wa nchi mbili yaani Burundi na Australia hadi sasa.
Miezi miwili baadaye, alikubali wito wa kikosi cha muda cha timu ya taifa ya Burundi kabla ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya 2019.Alicheza kwa mara ya kwanza 17 Juni 2019 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Tunisia katika kikosi cha kwanza.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Elvis Kamsoba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |