Ethiopia Habtemariam
Ethiopia Habtemariam (alizaliwa Berkeley, jimbo la California, 24 Septemba 1979) ni mkurugenzi mtendaji wa Rekodi ya Motown[1].
Maisha
haririMwaka 1994, alipokuwa na miaka 14, Habtemariam alianza kufanya kazi na Rekodi ya LaFace, lebo ya rekodi ambayo iliundwa na LA Reid, mkurugenzi mtendaji wa zamani wa Rekodi ya Epic. Kazi hiyo ilidumu kwa miaka minne. Baadaye, Habtemariam alifanya kazi na Kikundi cha Musiki ya Universal.
Mwaka 2011, Habtemariam alikuwa Makamu wa Rais Mwandamizi wa rekodi ya Motown. Yeye amefanya kazi na wanamuziki kama Stevie Wonder, Erykah Badu, Ne-Yo, Kem, BJ the Chicago Kid, Stacey Barthe, na wengineo.
Mwaka 2013, jarida la Mwanadishi ya Hollywood “Wanawake Katika Muziki” na Jarida la Variety alimwongeza Habtemariam kwenye orodha ya heshima iliyoitwa orodha ya athari za wanawake. Mwaka 2014, Habtemariam alikuwa Rais wa Rekodi ya Motown na hadi mwaka 2021 bado ni rais. Habtemariam ametumia urithi wa Motown kusaidia lebo hiyo nje ya orodha ya wasanii wa kurekodi. Mwaka 2017, alijiunga na muuzaji wa mavazi ya riadha Finish Line, na mwaka 2019, Motown alitengeneza wimbo wa matangazo kwa mtendaji wa NBA. Habtemariam alitengeneza wimbo wa sauti wa Queen & Slim pamoja na mkurugenzi wa filamu Melina Matsoukas na mwandishi wa skrini Lena Waithe. Mradi huo ulikuwa wimbo wa kwanza wa sauti wa Motown ukiongozwa na timu ya wanawake wote, kulingana na Billboard.
Habtemariam alipokuwa na miaka 16, aliandika kiandiko mpaka Sylvia Rhone. Yeye alifurahi na kushangaa ukweli kwamba mwanamke Mweusi alikuwa mwenyekiti wa lebo kuu ya kurekodi. Wakati Habtemariam alipokuwa mkuu wa rekodi, alipokea kiandiko kama hicho. Shibaki, mwanafunzi wa miaka 16 aliyejiunga na programu ya muziki ya Bonus Tracks, aliandika kuhusu juu ya jinsi mwanamke mweusi ako katika nafasi ya nguvu alivyokuwa akiwashawishi wanafunzi wachanga wa rangi.
Wakati alipofanya kazi katika LaFace, Habtemariam aliwaona wanawake katika nafasi ya nguvu na yeye alisema kwamba walimshawishi kusaidia wanawake vijana ili waje katika nafasi za nguvu. "Nilisikia watu wakisema, 'Oh, amepata kazi hiyo kwa sababu tu yeye ni mwanamke Mweusi na wanajaribu tu kutoa visingizio'. Sawa, poa. Hata ikiwa ndivyo ilivyokuwa, ni juu yangu. Je! Nitafanya nini ili kuathiri na kuwahakikishia watu wengine kupata fursa za aina hii baadaye? Isitoshe, ninapenda kuwaonyesha watu makosa”. Yeye anataka kusaidia wanawake vijana na kuwa na msaada kwa familia na jamii lake.[2][3]
Tanbihi
hariri- ↑ "Ethiopia Habtemariam Promoted to Motown Records Chairman/CEO". Billboard.com. Iliwekwa mnamo 1 Machi 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Meet the Music Mogul Bringing Motown Back". InStyle.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-25. Iliwekwa mnamo 2019-04-30.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help) - ↑ "How Ethiopia Habtemariam Became Universal Music Group's Most Powerful African-American Woman: 'I Love Proving People Wrong'". Billboard. Iliwekwa mnamo 2019-04-30.