Eugène Bertrand
Eugène Bertrand (15 Januari 1834 – 30 Desemba 1899) alikuwa mchekeshaji, mkurugenzi wa sanaa ya maigizo, na mkurugenzi wa nyumba ya opera wa Ufaransa.[1]
Maisha
haririEugène Bertrand alizaliwa jijini Paris na alifanya maonyesho yake ya kwanza kwenye Théâtre des Jeunes-Artistes kisha Théâtre de l'Odéon mjini Paris. Kuanzia mwaka 1859 hadi 1865, alifanya kazi kama mchekeshaji na mkurugenzi wa sanaa ya maigizo Marekani. Mwaka 1865, alikodishwa kwenye Théâtre du Parc mjini Brussels, kabla ya kusimamia kwa muda kumbi mbiili za michezo huko Lille (kaskazini mwa Ufaransa). Baadaye, alikua mkurugenzi wa Théâtre des Variétés kutoka mwaka 1869 hadi 1891.
Alikuwa mkurugenzi wa Opéra Garnier kuanzia tarehe 1 Januari 1892 hadi kifo chake mnamo mwaka 1899, kwanza kwa ushirikiano na Campocasso, na baadaye kuanzia mwaka 1894, na Pedro[2] Gailhard. Katika Opéra, alikua wa kwanza kwa mafanikio kutoa operas za Richard Wagner na pia aliandaa upya uzinduzi wa Samson et Dalila ya Saint-Saëns (1892) na kutoa mara ya kwanza maonyesho ya Thaïs ya Massenet (1894).[3]
Marejeo
hariri- ↑ "Eugène Bertrand" Ilihifadhiwa 10 Novemba 2017 kwenye Wayback Machine. at the artlyrique.fr website, accessed 4 May 2016.
- ↑ Les lettres reçues par lui dans ses différentes fonctions conservées aux Archives nationales sous les cotes AB XIX 4127 à 4129 (Voir la notice dans la salle des inventaires virtuelle des Archives nationales)
- ↑ Forman 2010, pp. 51–52.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Eugène Bertrand kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |