Eulalie Nibizi
Eulalie Nibizi (alizaliwa 1960) ni mwanaharakati wa vyama vya wafanyakazi nchini Burundi na mwanaharakati wa haki za binadamu. Mnamo 1991, alichangia kuanzishwa kwa chama cha kwanza cha wafanyikazi nchini Burundi, Union des travailleurs du Burundi, na kuendelea na kuanzisha chama cha walimu Syndicat des Travailleurs de l’Enseignement du Burundi. Mnamo mwaka wa 2015, akiwa Denmark, alipata habari kuwa mamlaka ya Burundi walikuwa wakimchukulia kama mwasi. Aliamua kwamba ilikuwa bora kutorudi katika nchi yake, ameishi uhamishoni tangu wakati huo. Tangu wakati huo Nibizi ameripoti kwa Umoja wa Mataifa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu nchini Burundi. Kama mratibu wa shirika la haki za binadamu Coalition Burundaise des Défenseurs des Droits de l'Homme, anaendelea kupigania maendeleo ya haki za binadamu kwa Warundi wote.[1][2][3]
Eulalie Nibizi | |
---|---|
Alizaliwa | 1960 |
Nchi | Burundi |
Kazi yake | Mwanaharakati wa haki za binadamu |
Marejeo
hariri- ↑ "| 50 ans après, PORTRAITS | Eulalie Nibizi ou la lutte pour la justice sociale – IWACU". www.iwacu-burundi.org. Iliwekwa mnamo 2022-03-24.
- ↑ "Defender of the month: Eulalie Nibizi – DefendDefenders" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-03-24.
- ↑ "Burundi: in state of fear, education union is targeted by government violence". Education International (kwa Kiingereza). 2015-12-14. Iliwekwa mnamo 2022-03-24.