Chama ni kikundi cha watu wanaoungana kwa lengo la kushirikiana ili kufikia lengo fulani, ambalo linaweza kuwa la aina nyingi tofauti, kwa mfano: dini, elimu, siasa, sanaa, michezo n.k.

Idadi ya wanachama inaweza kuwa tofauti sana, kuanzia wachache hadi milioni kadhaa.