Event:MUM Edithon
MUM Edithon
Muda wa kuanza na kumaliza
Mahali
Morogoro Tanzania
Jiunge na kikundi cha gumzo la tukio
Habari zenu wana Wikipedia,
Katika kuunga mkono juhudi za Wikimedia Foundation kupitia kampeni ya Wikilove Africa, tunakuletea Edit-a-thon kupitia Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) mnamo Oktoba 2024. Tukio hili la siku mbili litaandaliwa kwa lengo la kuongeza uelewa na ushiriki katika miradi ya Wikimedia, hasa Wikipedia.
Katika Edit-a-thon hii, tutatoa mafunzo kwa washiriki kuhusu:
- Wikipedia ni nini: Historia ya Wikipedia, maadili yake, na umuhimu wake katika kutoa maarifa kwa umma kupitia mtandao.
- Mwanzilishi wa Wikipedia: Historia ya kuanzishwa kwa Wikipedia na jinsi ilivyokua kuwa rasilimali muhimu duniani.
- Jinsi ya Kushiriki: Mchakato wa kujiandikisha kama mchangiaji, kuhariri makala, kuchangia katika Wikipedia.
- Mafunzo kwa Vitendo: Kuonyesha kwa vitendo jinsi ya kuwa sehemu ya jamii ya Wikipedia kwa njia rahisi na isiyo na changamoto.
Kwa kuongezea katika mafunzo ya jumla, tutajikita zaidi katika kuandika makala kuhusu Afrika, ikichukua maeneo ya msingi kama:
- Afya: Makala juu ya mifumo ya utoaji huduma ya afya, magonjwa, na mipango inayohusu uendelezwaji wa sekta ya afya Afrika.
- Elimu: Itatazamia mifumo na taasisi za elimu, sera, na mafanikio ya elimu ya Afrika.
- Miundombinu: Maelezo ya kina juu ya usafirishaji, mawasiliano, na kazi zote zenye kuleta maendeleo kwa umma wote wa Afrika.
- Siasa: Itatazamia mifumo ya kisiasas, viongozi, na matukio ya kihistoria ya mataifa ya Afrika.
- Maendeleo: Ukaguaji wa maendeleo ya kiuchumi, misaada ya kimatafaifa, na ukuaji wa maendeleo barani Afrika.
Wawezeshaji na Walimu
hariri- Wawezeshaji: Muddyb, Iddy Ninga, na Aneth (au mtu mwingine yeyote anayefaa kama Aneth ratiba zake zitabadilika). Pia watakuwepo wanawakipedia ya Morogoro iwapo wakakti utawaruzuku.
- Walimu: Watatu kutoka MUM (Watatoa mafunzo na usaidizi wakati wa mafunzo na mazoezi).
Hii ni mipango ya awali kwa ajili ya Edit-a-thon na itakuwa na manufaa kwa washiriki wote kwa kuimarisha uelewa wao na uwezo wa kuchangia kwenye Wikipedia. Ikiwa kuna maswali au maoni, tafadhali yachangie kwa ajili ya kuboresha mipango hii.