Fes
(Elekezwa kutoka Fès)
Fes (pia: Fez; Kiarabu: فاس)ni mji mkubwa wa tatu nchini Moroko baada ya Casablanca na Rabat. Kuna wakazi 946,815 (2004).
Mji ulianzishwa na mfalme Idris I mwaka 789. Tangu 859 Chuo Kikuu cha Al-Qairawin kilianzishwa. Baada ya mwisho wa himaya ya Waarabu katika Hispania Waislamu wengi kutoka kule walihamia Fes.
Tangu 1548 mji ulikuwa sehemu ya ufalme wa Moroko pia mji mkuu hadi mwaka 1912.
"Medina" au mji wa kale wa Fes imepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.
-
Geti ya mji wa Kale „Bab-al-mansur“
-
Ukuta wa Medina
-
Mji wa Fes
-
Karahana ya kutia rangi kwenye vitambaa na ngozi 1
-
Karahana ya kutia rangi kwenye vitambaa na ngozi 2
-
Karahana ya kutia rangi kwenye vitambaa na ngozi 3
-
Medina ya Fes
-
Jioni kwenye medina