Faharasa (pia faharisi, kutoka Kiarabu: الفهرس al-faharas; kwa Kiingereza: glossary, index) ni orodha ya mada au majina yaliyomo katika kitabu pamoja na kurasa vinapopatikana.

Farahasa ya majina katika kitabu ya Kilatini.

Inataja pia orodha ya maneno pamoja na maelezo mafupi ya maana yake. Inaweza kukusanya maneno mapya au magumu ya kitabu ambayo yanaelezwa maana zake. Faharasa kwa maana hiyo inapatikana kwa kawaida katika kurasa za mwisho za kitabu.

Faharasa inaweza kutaja pia orodha ya yaliyomo inayopatikana mara nyingi kwenye kurasa za mwanzo za kitabu, lakini inategemea desturi ya lugha husika.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Faharasa kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.