Fanani
Fanani ni mtu ambaye anawasilisha kazi za fasihi kwa hadhira.
Kwa mfano, mwimbaji anawaimbia watu ukumbini, hivyo fanani ni mwimbaji kwani anawasilisha ujumbe aliokuwanao kwa jamii, na hadhira ni watu wanaomsikiliza mwanamuziki kwani hawa hupokea ujumbe kuhusu jambo fulani kutoka kwa fanani.
Mifano mingine ya fanani, pamoja na mwimbaji, ni mwigizaji, mtangazaji, msimuliaji n.k.
Sifa za fanani
hariri- Msimulizi wa hadithi pia huitwa mtambaji, fanani au mganaji.
- Huwa mchangamfu na mcheshi kwa hadhira yake ili kuwafanya wapendezwe na hadithi za utamaduni wa jamii yake.
- Anaifahamu hadhira yake vizuri na kusimulia kulingana na mapendeleo yao: wasichana au wavulana? vijana au wazee?
- Huwa na uwezo wa ufaraguni - uwezo wa kubadilisha sehemu fulani za sanaa bila kujifunga na muundo asilia.
- Mwenye kumbukumbu nzuri.
- Mwenye uwezo wa kuigiza kwa kutumia viungo vyake, uso (ishara-uso) na sauti (kiimbo)
- Mwenye uwezo wa kujenga taharuki kwa kusita kidogo ili kuvuta nadhari ya hadhira yake.
- Hushirikisha hadhira yake katika nyimbo n.k.
- Mlumbi hodari na mkwasi wa lugha.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fanani kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |