Fikayo Tomori
Fikayo Tomori (alizaliwa 19 Desemba 1997) ni mchezaji wa soka ambaye anacheza kama beki wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza iitwayo Chelsea F.C.
Kazi ya klabu
hariri2017-18: Mkopo klabu ya Hull City
haririTarehe 31 Agosti 2017, Tomori alijiunga na klabu ya Hull City kwa mkopo wa msimu mrefu. Alicheza kwa mara ya kwanza tarehe 13 Septemba 2017, katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Fulham.
2018-19: Mkopo klabu ya Derby County
haririTarehe 6 Agosti 2018, Tomori alijiunga na klabu ya Derby county kwa mkopo wa muda mrefu.Alicheza kwa mara ya kwanza tarehe 11 Agosti katika mechi waliyofungwa 1-4 dhidi ya Leeds United.
2019-: Kurudi Chelsea
haririKufuatia kumalizika kwa mkopo wake, Tomori alirudi Chelsea ambako alipewa jezi No. 29.Mnamo 31 Agosti 2019, Tomori alicheza kwa mara ya kwanza Chelsea dhidi ya Sheffield United, ambayo ilimaliza sare ya 2-2 huko Stamford Bridge[1].
Alifunga goli lake la kwanza katika klabu hiyo ya Chelsea mnamo 14 Septemba 2019, akifungua goli kutoka nje ya boksi, kwenye ushindi wa 5-2 dhidi ya Wolves.
Kazi ya kimataifa
haririTomori alistahili kuiwakilisha Nigeria katika kiwango cha kimataifa kupitia kwa wazazi wake, Canada kupitia kuzaliwa kwake huko Calgary na Uingereza kupitia malezi yake aliishi nchini tangu alipokuwa mtoto mchanga.
Timu ya vijana ya Canada
haririMnamo 27 Machi 2016, Tomori aliichezea Canada mashindano ya vijana wa chini ya miaka 20 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Uingereza.
Tanbihi
hariri- ↑ "Chelsea 2-2 Sheffield United". SkySports. 31 August 2019. Retrieved 31 August 2019.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fikayo Tomori kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |