Franz Lambert
Franz Lambert (amezaliwa tar. 11 Machi 1948 mjini Heppenheim, Ujerumani) ni mtunzi na mpiga organ kutoka nchini Ujerumani. Anependa sana kupiga organ ya Hammond lakini pia alifahamika zaidi baadaye kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga Wersi ambayo ni organ ya umeme wakati wa shughuli zake na kutweza kutoa zaidi ya albamu 100.
Kujulikana kwake kwa mara ya kwanza katika umma ni baada ya kuonekana mnamo 1969 kwenye kipindi cha TV cha Kijerumani almaarufu kama Zum Blauen Bock, baada ya hapo akapata mkataba wake wa kuanzisha shughuli zake rasmi kwa mara ya kwanza. Amecheza na watu mashuhuri kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na Prince Charles na Helmut Schmidt.
Miongoni mwa kazi zake mashuhuri ni pamoja na FIFA Anthem, ambayo ilianza kupigwa kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia la FIFA 1994. Ikaendelea kupigwa kwenye kila michezo iliyoandaliwa na FIFA na michuano mingine ya timu zikijipanga kupiga kambi.
Anaishi mjini Heppenheim-Sonderbach, Hesse.
Tazama pia
haririViungo vya Nje
hariri- www.franzlambert.de Ilihifadhiwa 28 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine. (English)
- "Franz Lambert Demo Part 1" — 40 years on stage (Euro Tour 2005) YouTube
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Franz Lambert kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |