Fredricka Whitfield
Fredricka Whitfield (alizaliwa 31 Mei, 1965) ni mwandishi na mtangazaji wa habari. Anatangaza weekend edition ya chumba cha habari cha CNN kutoka makao makuu ya dunia huko Atlanta.[1]
Fredricka Whitfield | |
Nchi | Marekani |
---|---|
Kazi yake | Mwandishi |
Cheo | mwandishi wa habari |
Maisha ya mwanzo na elimu
haririWhitfield ni binti wa mwanariadha wa Marekani aliyeshiriki wa Olimpiki Mal Whitfield, aliyefariki tarehe 18 Novemba 2015.[2].[3]
Whitfield amesoma kwenye shule ya Paint Branch High School huko Burtonsville, Maryland,akahitimu mnamo mwaka 1983. Akapata shahada ya uandishi wa habari kutoka chuo kikuu cha Howard shule ya mawasiliano mnamo mwaka 1987.Wakati akiwa chuoni hapo aliwahi kuwa mtangazaji wa habari kwenye stesheni WHUR ya redio ya chuoni hapo. Mnamo mwaka 2002, Whitfield alichaguliwa kuonyesha mchango wake kama mwanafunzi wa zamani wa Howard.[1]
Kazi
haririBaada ya kuhitimu, Whitfield alifanya kazi kwenye stesheni ya televisheni ya WPLG huko Miami, News Channel 8 huko Washington, D.C., stesheni ya televisheni, ya KTVTin huko Dallas, WTNH huko New Haven, Connecticut,na WCIV huko Charleston,Carolina ya kusini.Kisha akafanya kazi na NBC News, akiwa kama muandishi huko Atlanta wa habari za usiku kwanzi mwaka 1995 mpaka 2001. Pia alifanya kazi kwenye vitengo vingine vya habari akiwa na NBC ikiwemo Today NBC program; akiwa kama msomaji wa habari za asubuhi na mchana pamoja na kuwa muandishi wa kazi mbalimbali.
Whitfield alianza kufanya kazi na CNN mnamo mwaka 2002, na amepitia habari kuu kadhaa. Alikuwa mwanahabari wa kwanza kutoa taarifa a kifo cha Ronald Reagan. Amehabarisha pia kuhusiana na tetemeko kwenye bahari ya hindi ya na sunami ya bara la Asia iliyotokea disemba mwaka 2004. Whitfield pia alihabarisha kutokea mji wa Persian Gulf wakati wa operesheni ya kutafuta uhuru huko Iraqi.
Whitfield kwa sasa anatangaza habari kutoka chumba cha habari cha CNN kwenye kipindi cha weekend edition makao makuu huko Atlanta.[1]
Maisha binafsi
haririWhitfield aliolewa na John Glenn, mkurugenzi wa upigaji picha kampuni ya The Atlanta Journal-Constitution, tangu mwaka 1999. Akapata mtoto wa kiume Januari mwaka 2005, akapata mapacha Novemba mwaka 2012 wa jinsia tofauti: wa kike anaitwa Nola na wa kiume anaitwa Gilbert.
Mabishano
haririMnamo mwaka 2014, Whitfield alikuwa na mahojiano na mchekeshaji Joan Rivers ambayo yalifikia mwisho ghafla baada ya Whitfield kupendekeza kuwa chekesho la Rivers inachochea ukatili na kumkosoa kwa yeye kuvaa nguo ya manyoya ya zabibu.[4] Whitfield alitambua mabishano hayo kwenye matangazo yaliyofuata, akiita nafasi yake ya mahojiano na Rivers kuwa mahojiano yaliyoongelewa mara nyingi zaidi.[5]
Tarehe 13 Juni 2015, Whitfield alimuelezea mnyang'anyi aliyevamia kituo cha polisi cha Dallas huko Texas, kama mtu jasiri, akimdhania kuwa mmoja wa magaidi. Siku iliyofuata alidai alikosea kuzungumza japo hakuomba msamaha rasmi.[6] Siku mbili baadae aliomba msamaha rasmi kuwa alitumia maneno yake vibaya na anaomba radhi sana.[7]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 "CNN Profiles - Fredricka Whitfield - Anchor". CNN.
- ↑ Darci Miller (Novemba 19, 2015). "Three-Time Olympic Track Champion Mal Whitfield Dies at 91". Team USA. Iliwekwa mnamo Januari 11, 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Navy SEALs in Afghanistan; Dance fever". CNN. Julai 6, 2005. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-17. Iliwekwa mnamo Januari 11, 2020.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Yahr, Emily. "Joan Rivers storms out of CNN interview, but was she genuinely upset?", The Washington Post, July 7, 2014.
- ↑ "Israeli Forces Raid Missile Site in Gaza; Germany Vs. Argentina for the World Cup; Flight Diverted to Remote Island Due to Odor; Winter Fun in the Desert; John Walsh Launches New Show On CNN; World Cup Fever Still Alive in U.S.", CNN, July 13, 2014.
- ↑ Josh Feldman. "CNN Anchor Offers On-Air Explanation for Calling Dallas Attack "Brave"", The Hollywood Reporter, June 14, 2015.
- ↑ "CNN anchor apologizes a second time for 'offensive' remarks". KDFW. Juni 15, 2015. Iliwekwa mnamo Januari 11, 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fredricka Whitfield kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |