Freeman Mbowe

Freeman Aikaeli Mbowe (amezaliwa 14 Septemba 1961) ni mwanasiasa Mtanzania, mwanachama na mwenyekiti wa Chama cha kisiasa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alichaguliwa tangu mwaka 2000 kuwa mbunge wa Jimbo la Hai lililopo mkoa wa Kilimanjaro, akarudishwa kwa miaka 20152020. [1] [2]

Alikuwa mmoja wa waasisi wa CHADEMA mwaka 1992, Mbowe anafahamika kuwa mpangaji mahiri wa mikakati, na hivyo kumfanya kuwa mmoja wa wapanga mikakati wakuu wa CHADEMA na kiongozi wa juu kabisa.[3] Mnamo mwaka 2005 Mbowe aliwania uraisi wa Tanzania kupitia chama chake cha CHADEMA na kuambulia alilimia 5.88 ya kura zote. [4]

Mnamo Julai 2021, Freeman Mbowe, alikamatwa pamoja na wanachama wengine kumi wa chama waliondoka kwenda Mwanza (kaskazini magharibi) ambapo walikuwa wakipanga mkutano.

MarejeoEdit