Mkoa wa Kilimanjaro

Mkoa wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 25000[1].

Mkoa wa Kilimanjaro
Mahali pa Mkoa wa Kilimanjaro katika nchi ya Tanzania
Mahali pa Mkoa wa Kilimanjaro katika nchi ya Tanzania
Majiranukta: 3°20′S 37°20′E / 3.333°S 37.333°E / -3.333; 37.333
Nchi Tanzania
Wilaya 7
Mji mkuu Moshi
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa
Eneo
 - Mkoa 13,209 km²
Idadi ya wakazi (2012)
 - 1,640,087
Tovuti: http://www.kilimanjaro.go.tz/

Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kupita yote barani Afrika, umo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. Jina la mlima huu ndilo limeupatia mkoa jina lake.

Mkoa wa Kilimanjaro umepakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa kusini na mikoa ya Manyara na Arusha upande wa magharibi.

WakaziEdit

Mkoani Kilimanjaro kuna wakazi wapatao 1,640,087 (sensa ya mwaka 2012).

Makabila makubwa mkoani humo ni Wachagga, Wagweno na Wapare, ambapo pia kuna makabila mengine madogomadogo kama Wamasai na Wakamba.

Makao makuu ya mkoa huu ni Moshi.

Katika sekta ya elimu wakazi wameendelea kidogo kwa maeneo ya mjini, lakini katika sehemu za vijijini elimu bado inatetereka kwa kiasi kikubwa, maana teknolojia ya utandawazi katika eneo kubwa haijashamiri.

WilayaEdit

Mkoa wa Kilimanjaro una wilaya 7 ambazo ni: Hai, Mwanga, Moshi mjini, Moshi vijijini, Rombo na Same na ile mpya ya Siha.

Majimbo ya bungeEdit

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Kilimanjaro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.