Fuko
Fuko mashariki (Tachyoryctes splendens)
Fuko mashariki (Tachyoryctes splendens)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Familia: Spalacidae (Wanyama walio na mnasaba na fuko vipofu)
Gray, 1821
Ngazi za chini

Nusufamilia 3:
Myospalacinae (Zokori) Lilljeborg, 1866
Rhizomyinae (Fuko-mizizi) Winge, 1887
Spalacinae (Fuko vipofu) Gray, 1821

Mafuko ni wanyama wa familia Spalacidae ambao wanachimba katika ardhi na kushinda takriban maisha yao yote chini ya uso wake. Wanyama wengine waitwao fuko ni wanafamilia wa Chrysochloridae (oda Afrosoricida), Bathyergidae (Rodentia), Talpidae (Soricomorpha) na Notoryctidae (Notoryctemorphia). Spalacidae za Afrika ziainishwa katika jenasi Tachyoryctes. Spishi zote hula mizizi, matunguu na viazi. Kwa hivyo wanyama hawa wana meno manne makubwa mbele mdomoni. Macho yao ni madogo au yamefunikika kwa ngozi, masikio ni madogo au yametoweka na mkia vilevile. Manyoya yao ni mafupi na magumu na yana rangi ya majivu, kahawia, hudhurungi au nyeupe.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri