Fukusi
Kidungadunga wa mchele (Sitophilus oryzae)
Kidungadunga wa mchele (Sitophilus oryzae)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Coleoptera (Wadudu wenye mabawa magumu)
Nusuoda: Polyphaga
Familia ya juu: Curculionoidea
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Familia 7:

Fukusi, vidungadunga au vipukusa ni wadudu wa familia ya juu Curculionoidea katika oda Coleoptera. Kuna familia 7 na moja, Curculionidae, ni baina ya familia kubwa kabisa yenye jenasi 6800 na spishi 83,000. Familia ya juu ina spishi 97,000. Pengine familia mbili nyingine zinatambuliwa, Platypodidae na Scolytidae, lakini siku hizi hupatiwa cheo cha nusufamilia, ijapokuwa njia ya maisha yao ya kupukusa katika ubao imegeuza umbo lao sana.

Maelezo hariri

Sifa bainifu ya fukusi ni domo refu lenye sehemu za kinywa kwenye ncha yake. Ukubwa wao unatofautiana kutoka mm 1 hadi 40. Vipapasio vya spishi nyingi sana vimepindika kama kisugudi, lakini fukusi wa kimsingi wana vipapasio nyofu.

Lava za fukusi hula tishu za mimea, miti au viyoga au mbegu zao. Wapevu hula maua, matunda, mbelewele, viyoga na kwa nadra wadudu, kama vile wadudu-gamba.

Kama chakula hariri

Lava za fukusi, zile kubwa hasa, huliwa mahali pengi pa dunia. Zinaweza kuliwa mbichi, zilizopikwa, zilizokaangwa au zilizobanikwa.

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki hariri

Picha hariri