Kukuziwa
Ndege wa maji wa familia Rallidae
(Elekezwa kutoka Fulica)
Kukuziwa | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 4 za kukuziwa: |
Kukuziwa ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia Rallidae. Wana mnasaba na viluwiri lakini ni ndege wa maji wa kweli (tazama shaunge pia). Wanaachana na viluwiri kwa kuwa na kigao kidogo juu ya domo. Rangi yao ni nyeusi au kijivu nzitu na mabawa ya spishi nyingi yana rangi ya kahawa. Rangi ya domo na kigao ni nyeupe au nyekundu. Vidole vyao vina ndewe, siyo ngozi kama mabata, ili kusogeza mbele kwa urahisi majini. Hula mimea, wanyama wadogo na mayai. Hujenga tago kubwa kwa mimea majini au ardhini na huyataga mayai 6-12.
Spishi za Afrika
hariri- Fulica atra, Kukuziwa Kigao-cheupe (Eurasian au Common Coot)
- Fulica cristata, Kukuziwa Pembe-nyekundu (Red-knobbed Coot)
- Fulica newtoni, Kukuziwa wa Morisi (Mascarene Coot) imekwisha sasa (kadiri ya 1700)
- Gallinula angulata, Kukuziwa Mdogo (Lesser Moorhen)
- Gallinula chloropus, Kukuziwa wa Kawaida (Common Moorhen)
- Gallinula comeri, Kukuziwa wa Kisiwa cha Gough (Gough Moorhen)
- Gallinula nesiotis, Kukuziwa wa Tristan da Cunha (Tristan Moorhen) imekwisha sasa
Spishi za mabara mengine
hariri- Fulica alai (Hawaiian Coot)
- Fulica americana (American Coot)
- Fulica ardesiaca (Andean Coot)
- Fulica armillata (Red-gartered Coot)
- Fulica caribaea (Caribbean Coot)
- Fulica cornuta (Horned Coot)
- Fulica gigantea (Giant Coot)
- Fulica leucoptera (White-winged Coot)
- Fulica rufifrons (Red-fronted Coot)
- Gallicrex cinerea (Watercock)
- Gallinula galeata (Common Gallinule)
- Gallinula melanops (Spot-flanked Gallinule)
- Gallinula pacifica (Samoan Wood Rail) (pengine inaainishwa katika jenasi Pareudiastes) labda imekwisha sasa
- Gallinula silvestris (Makira Moorhen) (pengine inaainishwa katika jenasi Pareudiastes au Edithornis) labda imekwisha sasa
- Gallinula tenebrosa (Dusky Moorhen)
- Tribonyx mortierii (Tasmanian Nativehen)
- Tribonyx ventralis (Black-tailed Nativehen)
Spishi za kabla ya historia
hariri- Fulica chathamensis (Chatham Island Coot) (mwisho wa Quaternary)
- Fulica infelix (Juntura, MMA, mwanzo wa Pliocene)
- Fulica prisca (New Zealand Coot) (mwisho wa Quaternary)
- Fulica shufeldti (Amerika ya Kaskazini, Pleistocene) – labda spishi ndogo ya Fulica americana
- Gallinula balcanica (Varshets, Bulgaria, kati ya Villafranchian)
- Gallinula hodgenorum (Hodgen's Waterhen) (New Zealand, mwisho wa Quaternary)
- Gallinula kansarum (Kansas, MMA, mwisho wa Pliocene)
- ?Gallinula sp. Viti Levu Gallinule (Fiji , mwisho wa Quaternary; labda Pareudiastes au jenasi mpya)
Picha
hariri-
Kukuziwa kigao-cheupe
-
Kukuziwa pembe-nyekundu
-
Kukuziwa wa kawaida na makinda
-
Kukuziwa wa Kisiwa cha Gough
-
Ngozi ya kukuziwa wa Tristan da Cunha ambaye amekwisha sasa
-
Hawaiian coot
-
American coot
-
Andean coot
-
Red-gartered coot
-
Caribbean coot
-
Horned coot
-
Giant coot
-
White-winged coot
-
Red-fronted coot
-
Watercock
-
Common gallinule
-
Spot-flanked gallinule
-
Dusky moorhen
-
Ngozi ya Samoan wood rail ambaye amekwisha sasa
-
Tasmanian native hen
-
Black-tailed native hen