Fungunyota (kwa Kiingereza star cluster) ni idadi ya nyota zinazokaa karibu katika anga-nje. Zinashikamana kwa nguvu ya graviti. [1] Fungunyota maarufu linaloonekana kwa macho ni Kilimia.

Fungunyota la Kilimia
Fungunyota tufe lenye jina la kisayansi Messier2 jinsi linavyoonekana kwa darubini

Kwa kutumia mitambo ya kisasa wataalamu wa astronomia wamekuta mafungunyota maelfu kadhaa lakini nyingi hazionekani kwa macho matupu au yanaonekana kama nyota ya kawaida tu.

Fungunyota ni tofauti na kundinyota. Katika kundinyota watu wanajumuisha nyota zinazoonekana kukaa karibu na kuwa na umbo maalumu wakitazama anga kwa macho, lakini hali halisi nyota hizo hazina uhusiano kati yao wala hazipo pamoja. Nyingine zipo karibu zaidi na Dunia na nyingine zipo mbali mno. Kinyume chake fungunyota ni kundi la nyota zilizopo karibu hali halisi.

Kwa jumla kuna aina mbili za fungunyota:

  • fungunyota la kawaida ambako kwa kawaida idadi ya nyota haizidi mamia kadhaa. Kilimia ni fungunyota la aina hii lakini ni kati ya nyota sita hadi tisa tu zinazoonekana kwa macho matupu kutegemeana na hali ya anga.
  • fungunyota tufe lina idadi ya nyota maelfu hadi milioni zinazokaa karibu kama tufe kubwa. Chache zao zinaonekana kama nyota kwa macho lakini nyingi zimeonekana tu tangu kupatikana kwa mitambo ya utazamaji ya kisasa.


Marejeo

  1. star cluster (astronomy) -- Britannica Online Encyclopedia. britannica.com. Iliwekwa mnamo 7 Aprili 2010.

Viungo vya nje

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fungunyota kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.