Gari la Nyayo ilikuwa mradi wa serikali ya Kenya wa kupanga na kutengeneza magari ya Kenya.

Magari ya Nyayo Kiwandani

Mradi huu ulianzishwa mwaka 1986 wakati rais Daniel Arap Moi aliomba Chuo Kikuu cha Nairobi kutengeneza magari.

Majaribio matano yalifanywa yaitwayo Pioneer Nyayo Cars na yalikuwa na kasi ya 120 km/h.

Shirika la magari la Nyayo liliundwa ili kuzalisha magari haya kwa wingi.

Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa fedha, magari haya hayakuingizwa katika uzalishaji.

Shirika la magari la Nyayo baadaye lilipewa jina la Numerical Machining Complex Limited, shirika la kuunda viungo vya chuma vya viwanda vingine.

Viungo vya nje hariri