Gastro-enterolojia
Gastro-enterolojia (kutoka Kigiriki kupitia Kiingereza gastro-enterology) ni tawi la elimu ya tiba linalohusu magonjwa ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Inaangalia ogani za mwili kuanzia mdomo hadi mkundu.
Magonjwa yanayoangaliwa mara kwa mara ni kwa mfano
- vidonda vya tumbo (gastric ulcers)
- kansa ya utumbo mpana (colorectal cancer)
- magonjwa ya ini kama kusinyaa kwa ini (pia sirosisi, ing. cirrhosis) na homa ya ini (pia: hepatitisi, ing. hepatitis)
- magonjwa ya utumbo kama vile ugonjwa wa siliaki, ugonjwa Crohn, vidonda vya utumbo mkubwa (ulcerative colitis)
- matatizo kama vile mvimbio (pia dispepsia, ing. dyspepsy), maumivu ya tumbo, utumbo tukutiko (colon irritabile).
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gastro-enterolojia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |