Gbenga Adeyinka
Ni mtangazaji wa televishini na redio, mchekeshaji na muigizaji kutokea Nigeria.
Gbenga Adeyinka (Alizaliwa 7 Mei 1968) ni mwigizaji, mchekeshaji, mtangazaji wa runinga, muandishi na mshereheshaji wa Nigeria aliyekulia Abeokuta, jimbo la Ogun huku akipenda kujiita kama mchekeshaji kinara wa Nigeria.[1]
Elimu
haririGbenga Adeyinka alisoma katika chuo kikuu cha Lagos, ambako alisomea lugha ya Kiingereza.[2]
Maisha binafsi
haririGbenga Adeyinka amemuoa Abiola Adeyinka, na wana watoto watatu.[3]
Maisha ya kazi
haririGbenga hufanya kazi ya kusherehesha katika sherehe nyingi za harusi hata nje ya Nigeria, na ndie mtu wa kwanza kuchapisha gazeti la vichekesho nchini Nigeria, liitwalo Laffmattazz.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.vanguardngr.com/2014/12/gbenga-adeyinka-versatile-mc-path-greatness/amp/
- ↑ Amagiya, Florence. "Gbenga Adeyinka: Versatile MC on the path of Greatness". vanguardngr.com. Vanguard Newspaper. Iliwekwa mnamo 21 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ezzina, Bosah. "Gbenga Adeyinka's Wife, Abiola Reflects On Her Life @ 50 + Their 21yr Marriage". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-01. Iliwekwa mnamo 21 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gbenga Adeyinka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |