Geneviève Waïte

Mwimbaji, mwigizaji kutoka Afrika Kusini

Geneviève Waïte (13 Februari 1948 - 18 Mei 2019) alikuwa mwigizaji, mwimbaji na mwanamitindo wa Afrika Kusini.[1]. Umaarufu wake wa uigizaji alikuwa mhusika mkuu katika filamu ya mwaka 1968 iliyofahamika kwa jina la Joanna.[2].Kama mwanamitindo, alipigwa picha ya Vogue magazine mnamo mwaka 1971 na Richard Avedon.[2] Na, mnamo mwaka 1974, alirekodi albamu yake ya pekee kama mwimbaji.[2]

Picha ya Geneviève Waïte

Maisha binafsi

hariri

Waïte aliolewa mara ya kwanza na Matthew Reich mnamo 10 Desemba 1968.[3]Baadaye, Waïte aliolewa na mwanamuziki John Phillips mnamo tarehe 31 Januari 1972.[2].Walikuwa na watoto wawili, waigizaji Tamerlane Phillips amezaliwa mwaka 1971 na Bijou Phillips amezaliwa mwaka 1980.[2] Waliachana mnamo mwaka 1985.Baadaye aliolewa na Norman Buntaine na baadaye walitengana.[3][4]

Muziki

hariri

Albamu ya Waïte ya mwaka 1974 Romance is on the Rise ilitengenezwa na mumewe wa pili John Phillips,zamani wa kikundi cha folk rock the Mamas & the Papas.Toleo la mwaka 2011 la albamu kwenye CD linamjumuisha toleo la Jalada ya wimbo wa Velvet Underground.[5]

Mnamo 18 Mei 2019, Waïte alikufa katika usingizi wake huko Los Angeles, California. Binti yake, Bijou, alitangaza kifo hicho siku kadhaa baadaye.

Marejeo

hariri
  1. "Geneviève Waïte". allmovie.com. Iliwekwa mnamo 17 Januari 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 "Geneviève Waïte, 71, Star of the Swinging-’60s Film ‘Joanna,’ Dies", The New York Times, The New York Times Company, 24 May 2019. Retrieved on 19 September 2020. 
  3. 3.0 3.1 "Geneviève Waïte". MyHeritage. Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "american female singer songwriters". Air Structures. Agosti 2004. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Oktoba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Genevieve Waite". Amazon Music. Amazon (company). Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Geneviève Waïte kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.