"Ghetto Gospel" ni wimbo wa rapa Tupac Shakur, ambo ulitolewa kama single ya pili baada ya kufa kwake. Wimbo unatoka katika albamu mwaka wa 2004, Loyal to the Game. Wimbo ulitungwa na Tupac Shakur ukiwa kama kilio cha "kumaliza vita mitaani", unalenga hasa utofauti wa ubaguzi wa rangu usio na maana na upingaji wa sera za haki za binadamu, hasa kwa wale walio-maskini mno. Wimbo umeshirikisha kibao cha Elton John cha Indian Sunset. Kwenye Ghetto Gospel 2pac anaelezea kinagaubaga kuhusu maisha ya watu wanaoishi ghetto. Wimbo umetayarishwa na Eminem. "Ghetto Gospel" ulikuwa wimbo pekee kutoka kwenye Loyal to the Game ukisindikizwa na muziki wa video. Mwishoni kabisa mwa video kuna ujumbe kutoka kwa mama'ke, Afeni Shakur, akisema "Kumbuka kujiweka hai, kwani hakuna muhimu zaidi ya hicho." Wimbo ulifikia nafasi ya #1 kwenye chati za UK, baada ya chini zaidi ya mwaka, rapa mhasimu The Notorious B.I.G. amefikia nafasi #1 na single yake ya Nasty Girl.
- CD single
Mtunzi (wa) | Sampuli |
1. |
"Ghetto Gospel" (akim. Elton John) | |
|
3:58 |
- UK CD single
Mtunzi (wa) | Mtayarishaji |
1. |
"Ghetto Gospel" (akim. Elton John) | | Eminem |
3:58 |
2. |
"Thugs Get Lonely Too" (akim. Nate Dogg) | | Eminem |
4:48 |
Pia kulikuwa na toleo ambalo hakumshirikisha Elton John.