Untouchable
"Untouchable" ni single iliyotolewa baada ya kufa kwa msanii wa muziki wa hip hop Tupac Shakur. Wimbo umemshirikisha msanii mwingine Krayzie Bone. Wimbo unatoka katika albamu ya Pac's Life. Wimbo ulitengenezewa reamixi yake na Swizz Beatz, ulikuwa wimbo wa pili wa kitaa kutolewa nyuma ya wimbo Pac's Life. Wimbo uliingia na kushika nafasi ya #91 kwenye chati za Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks na #21 kwenye chati za Hot R&B/Hip-Hop Singles -ulioanza kuuzwa mnamo tar. 2 Desemba 2006 toleo la jarida la Billboard. Mstari wa Tupac una mashairi sawa na yale ya kutoka katika nyimbo zingine kama vile Drunk freestyle, Killuminati na wimbo usiotolewa wa War Games. Nyimbo hizi zote zina mashairi sawa kwa sababu Tupac hakunuia kuzitoa au nyimbo za namna hii ziwe wazi. Mara kwa mara Tupac alikuwa akitumia nyimbo zisizotolewa kuwasawazisha mashairi yake ya sasa yawe vyema.
“Untouchable (Swizz Beatz Remix)” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya 2Pac akishirikiana na Bone Thugs-N-Harmony kutoka katika albamu ya Pac's Life | |||||
Imetolewa | 2006 | ||||
Muundo | CD, Vinyl | ||||
Aina | Gangsta rap | ||||
Urefu | 3:53 | ||||
Studio | Amaru/Interscope | ||||
Mtunzi | Tupac Shakur | ||||
Mtayarishaji | Swizz Beatz | ||||
Mwenendo wa single za 2Pac akishirikiana na Bone Thugs-N-Harmony | |||||
|
Makala hii kuhusu wimbo wa hip hop bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |