Yemen (kwa Kiarabu: ٱلْيَمَن‎, al-Yaman), rasmi Jamhuri ya Yemen, ni nchi iliyoko kwenye ncha ya kusini-magharibi ya Rasi ya Uarabuni barani Asia. Inapakana na Saudi Arabia kaskazini, Oman mashariki, na imepakana na Ghuba ya Aden na Bahari ya Shamu kusini na magharibi. Yemen ina eneo la takriban kilomita za mraba 555,000 na idadi ya watu inayokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 34. Mji wake mkuu ni Sana'a, ingawa serikali kwa sasa inaendesha shughuli nyingi kutoka mji wa muda wa Aden kutokana na hali ya kisiasa. Yemen ni mojawapo ya nchi zenye historia ndefu ya ustaarabu katika eneo la Kiarabu, ikiwa ni nyumbani kwa falme za kale kama Saba na Himyar.

الجمهورية اليمنية
Al-Jumhūriyyah al-Yamaniyyah

Jamhuri ya Yemen
Bendera ya Yemen Nembo ya Yemen
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Allah, al-Watan, at-Thawra, al-Wehda
(Mungu, taifa, mapinduzi, umoja)
Wimbo wa taifa: Jamhuri ya Maungano
Lokeshen ya Yemen
Mji mkuu Sana'a
15°21′ N 12°24′ E
Mji mkubwa nchini Sana'a
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali Jamhuri
Abd Rabbuh Mansur Hadi
Khaled Bahah
Establishment
Maungano ya Yemen Kaskazini
na Kusini

22 Mei 1990
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
527,970 km² (50)
kidogo sana
Idadi ya watu
 - Julai 2018 kadirio
 - 2004 sensa
 - Msongamano wa watu
 
28,498,683 (48)
19,685,000
44.7/km² (160)
Fedha Yemeni rial $1 = 198.13 Rials (YER)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+3)
(UTC)
Intaneti TLD .ye
Kodi ya simu +967

-


Hata hivyo, katika karne ya sasa, nchi hii imekumbwa na migogoro ya kisiasa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodhoofisha uchumi na hali ya kibinadamu.

Historia

hariri

Hadi mwaka 1990 palikuwa na nchi mbili za Yemen ya Kaskazini na Yemen ya Kusini.

Ile ya kaskazini ilikuwa Ufalme wa Yemen baada ya Imamu Yahya Muhamad wa kundi la Zaidiya kuvamia velayat ya Yemen ya milki ya Waturuki Waosmani (1 Novemba 1918). Baadaye ikawa Jamhuri kwa njia ya mapinduzi (1962).

Ile ya kusini ilikuwa sehemu koloni (Aden) na sehemu nchi lindwa (Hadramaut) ya Waingereza. Baada ya ukoloni kwisha ikawa mara moja Jamhuri (30 Novemba 1967).

Nchi hizo mbili ziliungana tarehe 22 Mei 1990, lakini uongozi ulizidisha ufisadi, na tangu mwaka 2011 hali ya siasa ni tata. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaendelea kwa misaada kutoka nchi za nje, hasa kutokana na uwepo wa makundi makubwa adui ya Wasuni na Washia.

Matokeo yake ni njaa kwa wakazi 17,000,000 kiasi kwamba Yemen imehesabika kuwa nchi inayohitaji zaidi misaada ya kibinadamu.

Wakazi wengi ni Waarabu wa makabila mbalimbali; wengine ni machotara wa Kiarabu-Kiafrika, Waajemi na Wazungu.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiarabu.

Upande wa dini, wananchi karibu wote (99%) ni Waislamu, wakiwemo Wasuni (60–65%) na Washia (35-40%). Waliobaki ni Wakristo, Wayahudi, Wahindu au hawana dini yote.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Yemen bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Yemen kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.