Girlfriend (filamu)

Girlfriend ni filamu iliyotoka mwaka 2003 nchini Tanzania.

Girlfriend

Posta ya Girlfriend
Imeongozwa na George Tyson
Imetayarishwa na Sultan Tamba
Kessa Mwambeleko
Imetungwa na Sultan Tamba
Nyota TID

Yvonne Cherryl
Jay Moe
King Crazy GK
A.Y.
Beatrice Morris

Muziki na P. Funk
Imehaririwa na Robert Kiata
Imesambazwa na GMC Wasanii Promoters
Imetolewa tar. 24, Mei, 2003
Nchi Tanzania
Lugha Kiswahili

Filamu inahusu muziki na maisha na ndani yake anakuja TID, Yvonne Cherrie (Monalisa), Beatris Morris (Nina), Jay Moe, A.Y na King Crazy GK. Filamu inaonesha jitihada binafsi katika kile unachokiamini na mwisho wa siku unatusua. Picha linaanza TID maisha magumu, harakati kila siku, huku ana mpenzi wake wa karibu mara kulala na njaa, mara hivi. Basi tu ilimradi maisha ya bahati nasibu. Hatimaye wakatoka katika namna ya kipekee licha ya majaribu kadhaa yaliyoonekana katika kipindi kigumu cha maisha yao. Filamu ina kibwagizo chake kinaitwa Girlfriend ambacho kiliimbwa na TID akishirikiana na Jay Moe kutoka Bongo Records.[1][2]

Hadithi

hariri

Filamu inaanza Eric (T.I.D) akiwa nyumbani anasikiliza Sister Sister ya King Crazy GK kwa zogo kubwa. Ghafula Zuena (Yvonne Cherrie) anaingia kuzima mazogo yale. Zeuna anamsihi mpenziwe atafute kazi ya kufanya na si hiyo ya muziki. Eric anaamini katika muziki na kamwe hawezi kuacha muziki. Zuena anaona muziki hauna faida yoyote kwa Eric, kwani hata kodi inamshinda kulipa. 

Mazungumzo yao hatimaye wakakubaliana kwenda pamoja katika kilabu ya muziki. Huko kilabuni, hakuwa kwenye ratiba, anabahatisha kutumbuiza. Kilabuni anaonekana Ndende, Jay Moe. Jahffarie, Sista P., G.K. anayebughudhi wasichana kilabuni hapo akiwa na A.Y. Stella (Nina) anamshawishi Zuena aachane na Eric kwa vile hana kitu. Bila mafanikio.

AY anamwona Zuena na kujaribu kumkuwadia GK. Eric bado hali mbaya katika kukubaliwa kutumbuiza. GK na AY wanarudi tena kuja kumbughudhi Zuena. Zuena anahofia nongwa na Eric na kuamua kuwatimua wawili wale. Kilabuni kunazuka ugomvi kila sehemu, GK na AY wanaleta fujo, hawataki kulipa pesa za vinywaji walivyokunywa. Hadi mwisho, Eric kabaniwa kutumbuiza kule kilabuni. Nyumbani kwa GK unatokea mzozo kati ya Stella na mwanamke mwengine (Joan). GK anagonganisha magari. 

Nyumbani kwa Sam (kakake Eric), malumbano makubwa ndani ya nyumba. Amekuwa kisirani kiasi hata mkewe anaoiona hiyo hali. 

Washiriki

hariri

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Girlfriend (filamu) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.