Khalid Mohamed (anafahamika zaidi kama T.I.D. yaani "Top in Dar"; amezaliwa Dar es Salaam, mwaka 1981) ni mwanamuziki wa Bongo Flava kutoka Tanzania.

Khalid Mohamed aka TID, 2015

Ameimba nyimbo nyingi maarufu nchini Tanzania. Kati ya nyimbo hizo ni Mrembo, Zeze, Girl Friend, Siamini na nyingine nyingi alizowahi kuimba na baadaye kuwa maarufu.

Maisha ya awali

hariri

TID alizaliwa kama Khalid na ni mtoto wa mwisho katika familia yao. TID alipata elimu ya msingi 1989 hadi 1996, na baadaye kumaliza elimu ya Sekondari mwaka 2000. Katika kipindi cha mwaka huohuo TID akawa anasomea masuala ya uhandishi kwa muda wa miezi minane na kuhitimu huku akichukua kozi ya kompyuta jijini Dar es Salaam.

Historia

hariri

TID alianza safari yake ya muziki mwaka 1994 akiwa na kundi la Black Gangsters, na baada ya miaka mitano akaanza kazi ya muziki kama msanii wa kujitegemea. Akiwa na umri wa miaka 21, alisaini mkataba na Poa Records na kuachia wimbo wake wa kwanza "Mrembo" mwezi Machi 2002. TID pia alicheza kama mhusika mkuu katika filamu "Girlfriend," inayohusu tasnia ya Bongo Flava.

Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni pamoja na "Kiuno," "Nyota Yako," "We Dada," "Zeze," na "Siamini." Amefanya maonyesho katika nchi za Afrika Mashariki, Uingereza, na Marekani, na huimba na bendi ya moja kwa moja iitwayo Top Band.

Kwa sasa, TID anaendelea na shughuli zake za muziki na anaweza kupatikana kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii kama Instagram na YouTube , ambapo anashirikisha kazi zake mpya na kuwasiliana na mashabiki wake.


Albamu Alizotoa

hariri

Sauti ya dhahabu aliyoshirikisha wasanii kama Jay Moe

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu TID kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.