George Tyson

George Tyson (jina la kuzaliwa George Otieno Okumu) (1973-2014) alikuwa muongozaji wa filamu kutoka Kenya. Alifanya kazi hasa nchini Tanzania. Alijulikana kwa kuongoza filamu kama Girlfriend na Dilemma. Tyson alifariki katika ajali ya gari tarehe 30 Mei, 2014 aliporudi kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam. Wakati wa kifo chake alikuwa na umri wa miaka 41. Girlfriend ilikuwa filamu yake iliyompa sifa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Filamu ilitayarishwa na Sultan Tamba na kusambazwa na GMC Wasanii Promoters.

MarejeoEdit

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu George Tyson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.