Girlfriend (wimbo wa Michael Jackson)

"Girlfriend" ni wimbo uliotungwa na Paul McCartney. McCartney alifikiria kwamba wimbo huu utamfaa Michael Jackson na anaweza kuupenda na kuurekodi, na alisema haya kwa Jackson wakiwa kwenye sherehe moja huko mjini Hollywood. Hata hivyo, McCartney aliishia kuurekodi mwenyewe akiwa na bendi ya Wings, na ukaja kutolewa mnamo mwaka wa 1978 kwenye albamu yao ya London Town.

“Girlfriend”
“Girlfriend” cover
Single ya Michael Jackson
kutoka katika albamu ya Off the Wall
B-side "Bless His Soul" (with The Jacksons)
Imetolewa Julai 1980
Muundo 7"
Imerekodiwa 1979
Aina Pop/R&B/Ballad
Urefu 3:05
Studio Epic Records
Mtunzi Paul McCartney
Mtayarishaji Quincy Jones
Mwenendo wa single za Michael Jackson
"She's out of My Life"
(1980)
"Girlfriend"
(1980)
"One Day in Your Life"
(1981)

Baadaye, ikaja kushauriwa na mtayarishaji Quincy Jones kwamba inawezekana ukawa kama mmoja kati nyimbo za Jackson kwa ajili ya albamu yake ya mwaka wa 1979, Off the Wall. Hata hivyo, Jones hakuwa anajua kama wimbo huu awali ulitungwa kwa ajili ya Jackson. Wimbo huu ulikuja kutolewa kama single mnamo mwaka wa 1980, katika UK pekee, ikiwa kama single ya tano na ya mwisho kutoka katika albamu ya Off the Wall album. Hii hakufanya vuzuri kabisa, iliweza kuingia kwenye chati ikiwa nafasi ya #41 na kutolewa kabisa kwenye chati hizo baada ya wiki tano.

Orodha ya nyimbo

hariri

UK single

hariri
  1. "Girlfriend" – 3:04
  2. "Bless His Soul" (akiwa na The Jacksons)

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Girlfriend (wimbo wa Michael Jackson) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.