Paul McCartney (alizaliwa 18 Juni 1942) ni mwanamuziki, mwimbaji, msanifu, mtunzi wa nyimbo na wa filamu Mwingereza aliyepata umaarufu wa kimataifa kama mwimbaji-mwenza na mcheza-gitaa ya besi wa The Beatles. Ushirikano wake na John Lennon katika uandishi wa muziki ndio uliofora zaidi kihistoria.

Paul McCartney jukwaani.

Baada ya the The Beatles kusambaratika mwaka wa 1970, Paul alijiendeleza kimuziki na akafora kivyake, akaiunda bendi The Wings na mkewe wa kwanza, Linda, pamoja na Denny Laine.

Kama mwanamuziki wa kujifunza, McCartney ana uwezo wa kucheza besi, gitaa, kibodi na ngoma. Anajulikana kwa mbinu yake ya kimelodia ya uchezaji wa besi (akiichezea sana kutumia kibonye, sauti yake ya tena ikiwa ya upana). McCartney alianza kazi yake ya kimziki akiwa na bendi ya the Quarrymen mwaka wa 1957, bendi ambayo ilibadilika kuwa the Beatles mwaka wa 1960. Kuanzia 1967, alianza uongozaji wa the Beatles na akawa meneja kibiashara wa bendi, akiipa motisha kufuatilia Bendi ya Stg. Pepper's Lonely Hearts Club. Katika nyimbo zake na the Beatles, "Yesterday" (1965) imeimbwa na wanamuziki 2,200 na zaidi, na imefanywa kihistoria kuwa mojawepo ya nyimbo zilizofora sana kupitia kuimbwa na wanamuziki wengine.

Mnamo 1970, aliiunda albamu ya kipekee McCartney. Kuanzia 1989, McCartney amekuwa akitembea kivyake.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paul McCartney kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.