Gladys Keitumetse Theresa Kokorwe[1] (amezaliwa Novemba 20 mwaka 1947)[2] ni mwanasiasa wa Botswana ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Kitaifa kutoka mwaka 2014 hadi mwaka 2019. Pia mwanachama wa Chama cha Kidemokrasia cha Botswana (BDP). [3]

Kabla ya kuingia katika siasa, Kokorwe alikuwa afisa wa umma wa ngazi ya juu. Alichaguliwa katika Bunge la Kitaifa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1994, na kutumikia kama waziri msaidizi katika serikali ya Festus Mogae kuanzia mwaka 1999 hadi 2004. Alikuwa naibu spika kuanzia mwaka 2004 hadi 2008, na kisha waziri katika serikali ya Ian Khama kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2009, ambapo aliondoka bungeni. Kokorwe alitumikia kama balozi wa Botswana nchini Zimbabwe kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2014, na kisha alirudi tena kwenye siasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2014, ambapo alikuwa mgombea mshindi wa BDP kwa nafasi ya spika.

Marejeo hariri

  1. "PAP Member Countries". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-12. Iliwekwa mnamo 2023-02-07. 
  2. "Typing her speaker's script". Mmegionline. 
  3. "100Women | Avance Media | Gladys Kokorwe" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-05-22. 
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gladys Kokorwe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.