Google My Business ni huduma ya mtandaoni kwa wamiliki wa kampuni za biashara inayoendeshwa na Google. Huduma hiyo ilizinduliwa mnamo Juni 2014[1] kama njia ya kuwapa wamiliki wa kampuni za biashara uwezo zaidi wa kuamua habari gani zionekane mtu anapotafuta jina fulani la biashara kwenye tovuti ya utafutaji ya Google.

Huduma hiyo inawawezesha watu kuthibitisha taarifa za biashara zao kama vile jina, anuani, n.k. Biashara zilizojisajili kwenye Google My Business hutokea pia kwenye Google Maps. Inasaidia pia biashara ndogo kupata wateja kupitia mtandao kwa kuwa matokeo ya utafutaji huonyesha aina za biashara zinazotafutwa katika makazi ya mtafutaji.

Maelezo ambayo hutokeza kwenye tovuti ya Google kutokana na huduma hiyo ni pamoja na saa za kufunguliwa kwa biashara, anuani, simu, na picha.[2][3]

Huduma hiyo hutolewa bure.[4]

Tovuti

Google My Business huwezesha wenye biashara kuunda tovuti zao bila gharama yoyote.[5]

Picha na video

Wamiliki wa biashara wanaweza kuweka picha na video kwenye ukurasa wao katika Google My Business.[6] Wanaweza pia kuweka nembo ya kampuni.

Marejeo

  1. Consultant, Ron Hanson, Post Bulletin Senior Media. A Brief History of Google My Business (en).
  2. Edit your business listing on Google. Iliwekwa mnamo 2019-03-02.
  3. How Google uses business information. Iliwekwa mnamo 2019-03-02.
  4. FAQs. Iliwekwa mnamo 2019-03-02.
  5. Create a free website for your business in minutes.. Iliwekwa mnamo 2019-03-02.
  6. Add local business photos or videos.

Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Google My Business kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.