Granada mpya

(Elekezwa kutoka Granada Mpya)

Granada mpya (Kihisp.: Virreinato de Nueva Granada) ilikuwa eneo la kikoloni la Hispania katika kaskazini ya Amerika Kusini kati ya 1717 na 1822. Leo hii nchi za Venezuela, Kolombia, Panama na Ekuador zimechukua nafasi yake.

Eneo la Granada mpya
Nembo la ufalme mdogo wa Granada mpya

Jina la Granada limetokana na mji wa Granada katika Hispania.

Granada mpya ilitawaliwa kama ufalme mdogo katika muundo wa Hispania. Gavana mkuu alikuwa na cheo cha mfalme mdogo (au: makamu wa mfalme).

Hadi 1717 ilikuwa sehemu ya ufalme mdogo wa Peru uliotawala Amerika Kusini ya Kihispania yote. Mji mkuu ulikuwa mwanzoni Cartagena na baadaye Santa Fé de Bogotá (leo Kolombia).

Nchi ya Kolombia iliendelea kutumia jina la Granada mpya hadi 1861.