Guguchawi
Maguguchawi ni mimea ya jenasi Striga katika familia Orobanchaceae iliyo vimelea. Guguchawi ni jina la jumla la spishi za Striga. Spishi kadhaa zina majina mengine, kama kakindu, kichaani, kichawi dume na kidevu cha mbuzi.
Mimea hii humelea manyasi hasa lakini spishi nyingine humelea jamiikunde. Mizizi yao ipenya mizizi ya mmea mlisha ili kuifyonzea maji na madini. Kwa hivyo inaweza kuleta hasara kubwa mashambani kwa muhindi, mtama, mwele, mkunde n.k.
Spishi za Afrika
hariri- S. aequinoctialis
- S. angolensis
- S. angustifolia
- S. asiatica, Kichawi Dume
- S. aspera
- S. bilabiata
- S. brachycalyx
- S. chrysantha
- S. dalzielii
- S. elegans, Kichaani
- S. forbesii
- S. gastonii
- S. gesnerioides
- S. gracillima
- S. hermonthica, Kichawi Dume
- S. hirsuta
- S. junodii
- S. klingii
- S. latericea
- S. lepidagathidis
- S. lutea
- S. macrantha
- S. passargei
- S. pinnatifida
- S. primuloides
- S. pubiflora, Kakindu au Kidevu cha Mbuzi
- S. yemenica
Picha
hariri-
Striga angustifolia
-
Striga asiatica
-
Striga bilabiata
-
Striga densiflora
-
Striga gesnerioides
-
Mche juu ya mizizi ya muhindi