Guru Granth Sahib (kwa Kipunjabi: ਸ਼੍ਰੀ ਗੁਰੂ ਗ੍ਰੰਥ ਸਾਹਿਬ ਜੀ gurū granth sāhib) au Adi Granth ni jina la kitabu kitakatifu cha dini ya Kalasinga (Usikhi).

Kalasinga akisoma Adi Granth katika Gurudwara.
Ukurasa wa nakala ya Adi Granth inayoonyesha ayat za Guru Gobind Singh; nakala hii ilitungwa mnamo karne ya 17 / 18.

Adi Granth inamaanisha "kitabu asilia". Guru Granth Sahib ni jina linaloeleza heshima kwa maandiko haya kama kiongozi wa kiroho: "Guru" ni cheo cha kiongozi wa kiroho, "Granth" ni "kitabu", na "Sahib" ni namna ya kumwita mkubwa kama "Bwana". Kwa hiyo kitabu hiki huheshimiwa kama kiongozi mkuu wa dini hii.

Yaliyomo ya kitabu ni ayat za nyimbo, sala na mafundisho yaliyotokana na maguru watano wa kwanza wa Kalasinga. Guru wa tano alikusanya ayat hizo na kuzipanga kama kitabu.

Guru wa kumi alithibitisha mkusanyo huu na kama mfuasi wake aliutangaza kuwa kiongozi wa jumuiya yote tarehe 7 Oktoba 1708.

Ayat zapangwa kwenye kurasa 1430.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.