Kizamiachaza
Kizamiachaza | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Vizamiachaza ni ndege wa jenasi Haematopus, jenasi pekee ya familia Haematopodidae. Ndege hawa ni weusi au weusi na weupe na wana domo na macho nyekundu na miguu pinki au myeupe. Huonekana pwani kwa kawaida ambapo hutafuta chakula wakiingiza domo lao kwa matope. Hula wanyamakombe, mwata, nyungunyungu na lava wa wadudu, pengine wanyama ngozi-miiba, kaa na samaki pia. Ndege wanaokula wanyamakombe wana domo lenye ncha nyembamba kama ubapa na hulitumia kulifungua kombe ikikata musuli wa mnyama. Wale wanaokula nyungunyungu wana domo kama msharasi. Hii ni kwa sababu ya uchakavu. Vizamiachaza hutaga mayai 2-4 chini ndani ya tundu ya kina kifupi.
Spishi za Afrika
hariri- Haematopus meadewaldoi, Kizamiachaza Mweusi wa Kanari (Canary Islands Oystercatcher) imekwisha sasa (1940?)
- Haematopus moquini, Kizamiachaza Mweusi (African Oystercatcher)
- Haematopus ostralegus, Kizamiachaza wa Ulaya (Eurasian Oystercatcher)
Spishi za mabara mengine
hariri- Haematopus ater (Blackish Oystercatcher)
- Haematopus bachmani (Black Oystercatcher)
- Haematopus chathamensis (Chatham Island Oystercatcher)
- Haematopus finschi (South Oystercatcher)
- Haematopus fuliginosus (Sooty Oystercatcher)
- Haematopus leucopodus (Magellanic Oystercatcher)
- Haematopus longirostris (Pied Oystercatcher)
- Haematopus palliatus (American Oystercatcher)
- Haematopus unicolor (Variable Oystercatcher)
Picha
hariri-
Kizamiachaza mweusi
-
Kizamiachaza wa Ulaya
-
Blackish oystercatcher
-
Black oystercatcher
-
South Island pied oystercatcher
-
Sooty oystercatcher
-
Pied oystercatcher
-
American oystercatcher
-
Variable oystercatcher