Mnyama Ngozi-miiba
Mnyama ngozi-miiba | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Nusufaila na ngeli:
|
Wanyama ngozi-miiba (kutoka Kiholanzi stekelhuidigen) ni wanyama wa bahari ambao wana ngozi yenye miiba na ulinganifu wa pembetano ingawa wahenga wao walikuwa na uwenzipacha. Hata lava wao wana uwenzipacha lakini hukuza pande tano wakiwa wazima. Mifano ya wanyama ngozi-miiba ni viti vya pweza, changa-maji, shashile, chani na kojojo.
Mwili wa wanyama ngozi-miiba una pande tano na umefunikika kwa ngozi yenye fuwele za kalsiti (kabonati ya kalisi) ziitwazo ossicles (vifupa). Kwa hivyo wanyama hawa wana aina ya kiunzi cha nje. Vifupa vya kiunzi hicho vimeunganika kabisa, kama kwa shashile na jamaa, au vimeunga kwa viungo, kama kwa viti vya pweza, changa-maji na kojojo. Katika matukio mengi vifupa hivyo vina michomozo kwa umbo la miiba, sugu au chembe (asili ya jina la faila hii).
Vineli vidogo vichomoza kupitia nyeleo za kiunzi. Kwa wanyama ngozi-miiba wengi hivi vinaweza kutumika kwa kusogea. Kwa wengine, kama mileli-bahari, hutumika kwa kukamata mawindo tu. Miguu hii ya neli (tube feet) inaweza kujishikiza chini au kwenye mawindo kwa njia ya mfyonzo.
Picha
hariri-
Mileli-bahari
-
Kiti cha pweza
-
Changa-maji
-
Chani
-
Kojojo
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mnyama Ngozi-miiba kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |