Hassan Dilunga
Mwanasoka wa Tanzania
Hassan Dilunga (alizaliwa 20.10 1993), ni mchezaji wa mpira wa miguu katika klabu ya Simba. Pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania au Taifa stars. Anacheza nafasi ya Kiungo mshambuliaji katika timu ya Simba.
Mafanikio ya mchezaji huyu: Alishawahi kucheza klabu bingwa Afrika, akiwa na timu yake ya Simba na kufikia hatua ya robo fainali na alifanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara akiwa na Simba.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hassan Dilunga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |