Hawara ni eneo la kihistoria katika Misri ya Kale lililopo kusini mwa Crocodilopolis (Arsinoe) kuelekea katika mteremko wa Oasisi ya Fayyum. Mgunduzi wa kwanza wa eneo hili alikuwa Karl Lepsius, mnamo mwaka 1843. William Flinders Petrie, alifika katika eneo hili kwa ajili ya uchunguzi mwaka 1888, pia walikuta karatasi za Mafunjo zilizotengenezwa na Wamisri ya karne ya kwanza na ya pili.Kwa Upande wa kaskazini mwa Piramid, kulikuwa na sehemu kubwa iliyokuwa na taswira za majeneza 146, iliyokuwa inakadiriwa kuwa katika eneo hilo tangu kipindi cha watu kutika Roma. Hii ikijulikana kuwa moja kati ya moja ya michoro ya zamani za kale iliyochorwa katika vitaby vya Roma

Piramidi ya Amenemhet III katika Hawara, Kutoka upande wa Mashariki

Amenemhet III aliyekuwa ndiye mtawala wa kinasaba mwenye nguvu zaidi wa Misri katika karne ya 12. Na pia lijenga piramidi katika eneo hili la Hawara. anasemekana kubadilisha tarehe za "Piramidi Nyeusi" iliyojengwa na yeye mwenyewe katika eneo la Dahshur. Katika eneo hili ndipo panaaminika kuwa ndiye sehemu aliyozikwa mtawala huyu. Pia katika eneo la Hawara ndipo kuna kaburi la Mtoto wa kike wa Amenemhet III aliyeitwa Neferu-Ptah, Kaburi hili lilipatika kiasi cha kilometa 2, kusini mwa piramidi la Mfalme.

Amenemhet III katika hekalu lake alilozikiwa katika makumbusho ya Cairo Misri

Katika hali ya kawaida, katika kipindi cha kati cha uongozi wa kifalme wa Misri Piramidi zilizojengwa baada taya Amenemhet II, ilikuwa ikijengwa kwa kutumia matope na mbao.Katika piramid hizo pia kulikuwa na sehemu kwa ajili ta kuzikia. Majengo mengine yaliyojengwa na mawe. Hii ikiwa ni staili ya kujenga ambayo hadi sasa hutumika katika majengo mengi nchini Misri. Hii leo, Piramidi nyingi zilizojengwa kwa kutumia matope na mbao yanaonekana kuharibika kutokana na mvua.

Wakati wa kuingia, kuna ngazi zinazoteremsha na kuingia katika chumba kidogo, na mbele kidogo kuna korido inayoingia ndani zaidi,. Juu ya korido hili kuna mlango wa kusukuma wenye uzito wa tani 20. kama mwizi akiwa anaingia katika jumba hili, baada ya kutoa mlango huu wa tani 20, mbele kidogo angekutana na mlango uliojengwa na kuni na matope mwizi huyo angehisi kuwa, alikuwa akipoteza muda kutoa mlango na hapo kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kukamatwa a walinzi.

Katika jumba hili ,kuna aina mbalimbali za ulinzi, lakini Pertie alikutahakuna haya mlango mmoja uliokuwa umefungwa, hii ikiwa na ile milango yenye uzitp wa tani kadhaa lakini hata ile milango ya miti. Hii inaweza ikiwa inaonesha uzembe wle waliofanya mazishi katika majumba hayo au pengine ni kutokana na kuwa na mategemeo ya kurudi hapo badae katika piramidi, au pengine ni nia ya makusudi ya kuwezesha wizi katika katika malkaburi, lakini kwa hali yote bado hakuna ushahidi wa kutosha kuhakikisha haya yote.

Sehemu ya mazishi ilikuwa imetengenezwa kwa kutumia nguzo ya jiwe, ambayo ilikuwa imeshushwa katika shimo ndani ya piramidi hiyo. Nguzo hii ilikuwa na uzito upatao tani 110 kwa mujibu wa Petrie. Maraba wa matofali ulipitishwa juu ya nguzo hii yam mawe na kuinua paa la sehemu hiyo na kufunikwa na vibamba vyenye kiasi cha uzito wa tani 45, .[1][2][3]

Njia ya kuingia katika piramidi hii leo imefurika na maji yenye kina cha mita sita, hii ni kutokana na maji kutoka katika mfreji wa Bahr el-Yusuf (Joseph's Canal) ambao unatiririka katika njia mbili na kupita katika mita 30 ndani ya piramidi.

Petrie hazina iliyozikwa mwaka 1911

Haekalu la kuekea maiti ambalo awali lilikuwa limesimama mkabala na piramidi hili, linaonekana kuwa, ndilo jengo lenye michoro mizuri inayojulikana kama "labyrinth" ilichorwa na Herodotus na pia imetajwa na Strabo na Diodorus Siculus.

Malkia Sobekneferu wa ufalme wa Misri wa kumi na mbili, amajenga katika eneo hili. Jina la malikia huyu linaamisha "Sobek nzuri kuliko yote",.

Moja kati ya ugunduzi uliofanywa na Flinders Petriealiweza kugundua nyaraka zmbalimbali, nyingine zikiwa zimeviringishwa. Na pia kuna nyingine ambazo zinatokeze katika kitabu cha Iliad toleo la kwanza na la pili.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Edwards, Dr. I.E.S.: The Pyramids of Egypt 1986/1947 p. 237-240
  2. http://www.touregypt.net/featurestories/amenemhet3hp.htm
  3. Siliotti, Alberto, Zahi Hawass, 1997 "Guide to the Pyramids of Egypt"

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hawara kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.