Gambamiti
(Elekezwa kutoka Hemirhagerrhis)
Gambamiti | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Gambamiti wa kawaida (Hemirhagerrhis nototaenia)
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Spishi 4:
|
Gambamiti ni spishi za nyoka wa jenasi Hemirhagerrhis katika familia Lamprophiidae. Mchana hupanda miti na vichaka ambapo huwinda mijusi na kula mayai yao. Juu ya gome la mti hawaonekani vizuri kwa ajili ya muungano wa rangi, madoa na milia (kamafleji, asili ya jina lao).
Chonge zao ni meno ya nyuma kabisa na mdomo ni mdogo. Kwa hivyo gambamiti sio hatari kwa watu. Waama wakikaribishwa hawasogei na wanategemea majificho yao.
Spishi
hariri- Hemirhagerrhis hildebrandtii Gambamiti Mashariki (Eastern bark snake)
- Hemirhagerrhis kelleri Gambamiti Milia (Striped bark snake)
- Hemirhagerrhis nototaenia Gambamiti wa Kawaida (Bark snake)
- Hemirhagerrhis viperina Gambamiti wa Angola (Western bark snake)
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gambamiti kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |