'

Hendry Kanje
Hendry Kanje
Amezaliwa(1993-03-05)Machi 5, 1993
NchiMtanzania
Majina mengineKanje
Kazi yakeMjasiriamali na mfanyabiashara


Hendry Ezekiel Kanje (amezaliwa wilaya ya Siha, mkoa wa Kilimanjaro, 5 Machi 1993) ni mjasiriamali na mfanyabiashara kijana kutoka nchini Tanzania. Kanje ni mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Trophacom na Digital Power Companies.[1]

Kanje amejikita zaidi katika uga wa nishati na maarifa juu ya vifaa vya umeme vya majumbani na viwandani. Kanje ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Iringa ambapo alipata shahada yake ya kwanza katika somo la biashara.[2]

Maisha ya awali hariri

Kanje alizaliwa na jina la Hendry Ezekiel Kanje alizaliwa mnamo tarehe 5 Machi, 1993, Siha Kilimanjaro Tanzania. Akiwa mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu. Mwanamume mmoja huku wanawake wakiwa wawili.

Baadaye katika elimu yake ya awali na kati alitumia muda wake mwingi akiwa katika Wilaya ya Siha. Baadaye akajiunga shule ya upili ya Muungano kati ya 2007-2010.

Hatua za chini zilipokamilika akajiunga kupata stashahada yake ya kwanza ya usimamizi wa biashara katika Chuo Kikuu cha Iringa kati ya 2016 - 2018.

Ujasiriamali hariri

 

Kanje awali alikuwa na moyo mkubwa wa kujitolea katika mbalimbali. Roho hiyo ikawa msingi hadidi wa kukuza maazimio anuwai ya kibiashara. Alijitolea kufanya kazi katika maeneno ya tabaka la chini nchini Tanzania akiwa na asasi za kimataifa. Alilenga hasa maeneo ya vijijini.

Mwaka wa 2014 alifanya kazi na Raleigh International kwa muda wa miezi mitatu kwa lengo la kuunga mkono harakati za mifumo ya maji, mradi wa kusafisha mikono na kujenga vyoo mashuleni katika mkoa wa Singida.

Baadaye akajiunga katika katka mradi wa 'Save the Children' uliofanyika Ndala Shinyanga na mwaka wa 2018 alirejea kufanya kazi tena na Raleigh International safari hii akiwa mjini Iringa katika Kijiji cha Lyamgungwe. Hapa alikuwa kama mkuu wa kikoksi cha kusaidia wajasiriamali wadogo waweze kufikia malengo ya miradi yao.

Pia amewahi kufanya kazi na asasi nyingine kama vile Voluntary Service Overseas (VSO) World Merit, Raleigh Tanzania Society na Gifted Heart Foundation.

Kwa upande wa uongozi, aliwahi kuwa mwenyekiti wa World Merit huko Iringa Region, mwenyekiti wa Raleigh Tanzania Society ana mkurugenzi wa mauzo katika Honle International kabla ya kuanzisha kampuni zake Digital Power na Trophacom huku akiwa mtendaji mkuu wa kwanza katika kampuni zote mbili.[3]

Biashara hariri

 
Kanje 2022.

Kanje alivutiwa kufanya biashara tangu akiwa bwana mdogo. Akiwa na umri wa miaka 11, alikuwa akihudumia wateja katika duka la mama yake mzazi. Akiwa anahudumia wateja wa mama yake, akaanzisha biashara yake mwenyewe ndogo ya kufunga pakiti za karanga katika ukubwa anuwai. Akawa anatumia duka la mamake kufanya biashara zake pia.[4]

Katika kufanya biashara hiyo ya karanga alichukulia kama kitu kidogo lakini ilisaidia sana kujenga ari ya kibiashara mtimani. Baada ya kumaliza elimu yake ya upili, akahamia jijini Mbeya kuendelea na masuala ya biashara. Akiwa huko, alitumia muda wake mwingi kuuza simu za mkononi na vifaa vyake kabla ya kurudi Himo Kilimanjaro na kujiunga na Tan Picture Universal Studio kwa ajili ya masomo mbalimbali ikiwa ni pamoja maigizo, stadi za maisha na masuala ya utamaduni.

Kupitia Tan Pictures na Universal Studio, alishawishika kujikita zaidi kwenye tasnia ya filamu. Wazo lake la kwanza ni kuwa mwigizaji maarufu katika tasnia ya filamu. Alianzisha kazi yake ya kwanza kwa ajili ya Filamu za Bongo akiwa na mnasihi wake Bwana Lucas Mkude ambaye alihakikisha anamkutanisha na hayati Ruge Mutahaba. Kutano hilo lilikuwa kujadili namna ya kujikwamua kimaisha kupitia sanaa ya uigizaji. Hata hivyo, wazo hili hakuendelea nalo.

Akiwa kama muuzaji wa kampuni ya Kichina ya Shenyang VPEC electrical, Kanje akapandishwa cheo. Akapewa fursa ya kuanzisha tawili lingine la kampuni huko Lusaka, Zambia na Maputo, Msumbiji. Lakini akakataa kazi hiyo na hatimaye kuanzisha biashara yake mwenyewe.

Kupitia Digital Power, Kanje anatoa maarifa anuwai kuhusu matumizi sahihi na chanya ya mitandao. Kwa kutumia uzoefu wake wa miaka mitano katika katika uuzaji na usambazaji wa vifaa vya umeme vya majumbani na viwandani, Hendry Kanje akajikuta akiungana na baadhi ya watu na kuanzisha Trophaco Africa.[5]

Marejeo hariri

  1. Sakata la wafanyabiashara ndogo ndogo (in sw-TZ), retrieved 2023-01-08 
  2. world youth skills day (in sw-TZ), retrieved 2023-01-08 
  3. Namna ya Kukuza Mtaji wako (in sw-TZ), retrieved 2023-01-08 
  4. “Baba Tajiri Baba Maskini” (in sw-TZ), retrieved 2023-01-08 
  5. Namna bora ya Kutangaza Biashara kwa Njia ya Mitandao (in sw-TZ), retrieved 2023-01-08 

Viungo vya Nje hariri