Wilaya ya Siha
Wilaya ya Siha ni mojawapo kati ya wilaya 7 za Mkoa wa Kilimanjaro yenye msimbo wa posta 25400.
Wilaya hii ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Hai.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 139,019 [1]. Wilaya ya Siha inakaliwa na wakazi wa makabila mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za nchi na nje ya nchi, wakiwemo wenyeji wa wilaya hiyo Wachagga (Wasiha).
Wasiha, kama walivyo Wachagga wengine, wakijihusisha na shughuli mbalimbali za uchumi, vikiwemo biashara, kilimo pamoja na ufugaji, ikiwa wanalima mazao makuu ya kahawa, ndizi, mahindi, maharage, viazi na mazao mengine ya biashara na chakula.
Wasiha wanasema moja kati ya lahaja nyingi za Kichagga zilizopo mkoa wa Kilimanjaro wakiwa na mchanganyiko na muingiliano mkubwa na lahaja ya Kimachame wakiwa ndio wenyeji halisi wa wilaya hiyo wakikaa na kuwekeza maisha yao kwa wingi upande wa kaskazini magharibi mwa wilaya hiyo. Lugha ya Wachagga wa Siha inalandana sana na ile ya Machame, hata hivyo hutofautiana kidogo sana kwenye matamshi na maana za maneno, ila wanaelewana kwa asilimia kubwa ukilinganisha na Wachagga wengine, hata majina wanayotumia mara kwa mara utayasikia yakilandana.
Wasiha kama walivyo Wachagga wengine pia, wana koo tawala ambazo ndizo koo zinazosikika zaidi. Koo hizo ndizo koo zilizotoa viongozi wa kitamaduni (Mangi) wa kabila hilo zikiwemo Kileo, Orio, Mmari, Mwandri, Munuo, na koo nyingine ndogondogo kama vile Mrang'u, Mosi, Maseri, Masaki. Ni nadra sana kusikia Mangi wa Siha ila kwa sasa Utawala wa Umangi unashikiliwa na ukoo wa Kileo.
Tanbihi
haririRamani | Wilaya au manisipaa | Wakazi (2022) | Tarafa | Kata | Kijiji | Eneo km² |
---|---|---|---|---|---|---|
Wilaya ya Hai | 240,999 | 17 | 1,217 | |||
Wilaya ya Moshi Vijijini | 535,803 | 32 | 1,300 | |||
Wilaya ya Moshi Mjini | 331,733 | 21 | 63 | |||
Wilaya ya Mwanga | 148,763 | 20 | 1,831 | |||
Wilaya ya Rombo | 275,314 | 28 | 1,471 | |||
Wilaya ya Same | 300,303 | 34 | 6,221 | |||
Wilaya ya Siha | 139,019 | 17 | 1,217 | |||
Jumla | 1,861,934 | 152 | 13,209 | |||
Wilaya ya Siha hii ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Hai. | ||||||
Marejeo: Mkoa wa Kilimanjaro |
Kata za Wilaya ya Siha - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ||
---|---|---|
Biriri | Donyomurwak | Gararagua | Ivaeny | Karansi | Kashashi | Kirua | Livishi | Makiwaru | Miti Mirefu | Nasai | Ndumeti | Ngarenairobi | Olkolili | Ormelili | Sanya Juu | Songu |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Siha kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|