Hessen-Marburg (kwa Kijerumani: Landgrafschaft Hessen-Marburg) ilikuwa utemi wa kihistoria nchini Ujerumani. Ilikuwa utemi wa kujitegemea ndani ya Dola Takatifu la Kiroma. Watawala wake walikuwa na cheo cha landgraf (ing. landgrave)

Utemi wa Hessen (buluu nyeupe), sehemu ya kusini ilikuwa Hessen-Marburg

Utemi wa Hessen ulianzishwa mnamo 1265 kwa kugawa utemi mkubwa wa Thuringia. Hessen-Marburg ilitokea kama nchi ya pekee wakati mtawala wa Hessen aligawa maeneo yake kati ya wana wake wawili kwenye mwaka 1458. Ilhali mtawala wa eneo alifariki bila mrithi, eneo likaunganishwa tena na Hessen kubwa.

Ugawaji wa pili ulitokea mnamo mwaka 1567 ukadumu hadi 1604. Baadaye iligawiwa tena kati ya temi za Hessen-Darmstadt na Hessen Kassel. Leo hii maeneo yake yamo ndani ya jimbo la Hesse la Ujerumani.

Maeneo yake yalikuwa na miji ya Marburg, Gießen, Nidda na Epstein pamoja na vijiji vya karibu.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hessen-Marburg kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.