Mtemi ni cheo cha mtawala wa kijadi hasa upande wa bara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye hapo zamani alitawala dola lenye mamlaka kamili katika nchi yenye watu hasa wa jamii moja. Mfano mmojawapo ni Mtemi Mirambo.

Mtemi Mirambo mwaka 1880

Etimolojia Edit

Neno mtemi au ntemi hutumiwa na lugha za makabila ya kati ya Tanzania, kwa mfano Kisukuma, Kinyamwezi na Kigogo likimaanisha mtawala, pia kwa Kibena huitwa Mtema, yote yakitokana na masdari ya Kibantu -tem-a, likimaanisha tawala.

Hakuna tafsiri ya moja kwa moja ya Kiswahili ya neno mtemi, hivyo lilikopwa kutoka lugha hizo kama lilivyo na kufasiriwa zaidi kimuktadha kwa kukosa tafsiri ya kisemantikia.

Kwa mfano:

  • Wakati wa majilio ya Waarabu na biashara ya utumwa lilifasiriwa kama Sultani
  • Wakati wa wamisionari na wapelelezi lilifasiriwa zaidi kama Sultani, Mfalme au Chifu kwa kuhusisha uwiano wa kidini, ukubwa wa milki na ushawishi wa kisiasa wa Watemi mbalimbali
  • Wakati wa ukoloni lilifasiriwa zaidi kama Chifu ili kuweka tofauti baina ya Mfalme wa Mabwana wa kikoloni na Watwana wa Kiafrika
  • Baada ya ukoloni hadi hivi sasa hufasiriwa zaidi kama Chifu au kuachwa lilivyo, Mtemi.
  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtemi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.