Kiongozi ni mtu ambaye huongoza kikundi cha watu. Mara nyingi kiongozi hupewa heshima ya juu katika jamii, kikundi cha watu au katika familia ambapo huheshimiwa na watu wote katika eneo husika analolisimamia kiongozi kwa ajili ya kuwaongoza watu.

Kiongozi katika jamiiEdit

Katika nchi nyingi duniani kiongozi hupatikana kwa wananchi kupiga kura ambapo watu mbalimbali wanaogombea uongozi hupigwa kura kwa ajili ya kuwa kiongozi katika jamii au kikundi cha watu hupatikana.

Mara nyingine kiongozi huchaguliwa kwa kuteuliwa na mtu mmoja pasipo kupigwa kura.

Pia katika jamii nyingine kiongozi hupatikana kwa kurithi, ambapo mrithi huwa kiongozi kwa kurithi uongozi kutoka kwa kiongozi aliyefariki na kuachia madaraka.

Kiongozi katika familiaEdit

Kiongozi katika familia huwa ni mtu aliye na umri mkubwa katika familia husika, ambapo viongozi huwa ni baba na mama. Katika familia nyingi baba ndio huwa kiongozi mkubwa akifuatiwa na mama.

Pia familia huweza kuwa na kiongozi wa ukoo ambapo bibi na babu huwa viongozi wa juu katika ukoo.

Kiongozi katika BibliaEdit

Katika Biblia kiongozi ni mtu ambaye huchaguliwa na Mungu kwa ajili ya kuongoza watu wake hapa duniani.