Hidrokaboni
Hidrokaboni ni aina mbalimbali za kampaundi ogania za kikemia zinazojengwa kwa atomi za hidrojeni na kaboni pekee.
Kwa asili zinapatikana hasa katika mafuta ya petroliamu iliyotokana na mchakato wa kuoza kwa mimea na mata ogania yenye kaboni na hidrojeni nyingi. Hidrokaboni haziwezi kuingia katika mmenyuko wa kikemia na maji.
Hidrokaboni ni chanzo muhimu cha nishati kwa binadamu duniani; petroli na diseli ni mchanganyiko wa aina za hidrokaboni.
Vikundi vya hidrokaboni
haririHidrokaboni hupangwa katika vikundi 5.
Alkani
haririAlkani ni hidrokaboni za msingi. Fomula yake ni CnH2n+2.
Jina la alkani | Fomula |
---|---|
Methani | CH4 |
Ethani | C2H6 |
Propani | C3H8 |
Butani | C4H10 |
Pentani | C5H12 |
Hexani | C6H14 |
Heptani | C7H16 |
Oktani | C8H18 |
Nonani | C9H20 |
Dekani | C10H22 |
Alkeni
haririAlkeni hufanana na alkani lakini zina muungo jozi kati ya kaboni na kaboni. Fomula yake ni CnH2n.
Jina la alkeni | Fomula |
---|---|
Etheni | C2H4 |
Propeni | C3H6 |
Buteni | C4H8 |
Penteni | C5H10 |
Hexeni | C6H12 |
Hepteni | C7H14 |
Okteni | C8H16 |
Noneni | C9H18 |
Deseni | C10H20 |
Alkini
haririAlkini zina muungo wa mara tatu kati ya kaboni na kaboni. Fomula yake ni CnH2n-2
Jina la alkini | Fomula |
---|---|
Ethini | C2H2 |
Propini | C3H4 |
Butini | C4H6 |
Pentini | C5H8 |
Hexini | C6H10 |
Heptini | C7H12 |
Octini | C8H14 |
Nonini | C9H16 |
Desini | C10H18 |
Sikloalkani
haririSikloalkani ni isomeri za alkeni. Fomula yake ni pia (CnH2n) lakini hazina muungo jozi kati ya kaboni na kaboni.
Jina la Sikloalkani | Fomula |
---|---|
Siklopropani | C3H6 |
Siklobutani | C4H8 |
Siklopentani | C5H10 |
Siklohexani | C6H12 |
Sikloheptani | C7H14 |
Sikloctani | C8H16 |
Siklononani | C9H18 |
Siklodekani | C10H20 |
Alkadini
haririAlkadini zina muungo jozi mbili kati ya kaboni na kaboni. Fomula ni CnH2n-2. Hizi ni isomeri za Alkini.
Hidrokaboni aromatiki
haririHidrokaboni aromatiki ni molekuli ogania yenye umbo la mviringo tambarare. Fomula yake ni CnH2n-6 na "n" ni sawa na kubwa kuliko 6.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hidrokaboni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |