Hifadhi ya Taifa ya Bui
Hifadhi ya taifa
Hifadhi ya Taifa ya Bui, inapatikana nchini Ghana ilianzishwa mnamo 1971. Eneo ni kilomita za mraba 1821. [1] Iko katika eneo la savana ya misitu. [2]
Hifadhi hiyo inajulikana kwa idadi kubwa ya viboko katika Volta Nyeusi. Tumbili aina ya colobus weusi na weupe na aina mbalimbali za swala na ndege wapo pia . [3] Sehemu ya hifadhi hiyo imefunikwa na hifadhi ya Bwawa la Bui, ambalo lilijengwa mnamo 2007 hadi 2013. [4]
Mahali
haririMbuga ya Taifa ya Bui imegawanywa na Mto Volta ; sehemu ya Magharibi ya mto ni sehemu ya eneo la Bono na sehemu ya Mashariki ya mto ni sehemu ya Mkoa wa Savannah wa Ghana . Hifadhi hiyo inapakana na Ivory Coast upande wa Magharibi. Miji ya karibu zaidi na hifadhi ni Nsawkaw, Wenchi na Techiman . [5] [6]
Marejeo
hariri- ↑ protected planet: Bui in Ghana Archived 12 Machi 2018 at the Wayback Machine.
- ↑ "Bui National Park, Ghana". www.oldwebsite.fcghana.org. Iliwekwa mnamo 2021-09-01.
- ↑ The Forest Commission of Ghana: Bui National Park, retrieved on May 7, 2011
- ↑ "Home". BUIPOWER (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-12-13.
- ↑ "Bui National Park". Ghana Wildlife Division. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Februari 2020. Iliwekwa mnamo 23 Aprili 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ WhiteOrange. "Brong Ahafo". Ghana Tourism Authority (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-06. Iliwekwa mnamo 2020-01-31.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |