Kodivaa[1] (kwa Kifaransa: Côte d'Ivoire[tanbihi 1], rasmi Jamhuri ya Kodivaa ni nchi ya Afrika ya Magharibi. Imepakana na Liberia na Guinea upande wa magharibi, Mali na Burkina Faso kaskazini, Ghana mashariki na Ghuba ya Guinea ya Atlantiki upande wa kusini. Ikiwa na idadi ya watu milioni 32 ni nchi ya 32 kubwa duniani kwa idadi ya watu. Yamoussoukro ndio mji mkuu na Abidjan ndio mji mkubwa.

Jamhuri ya Kodivaa
République de Côte d'Ivoire (Kifaransa)
Kaulimbiu:
Union – Discipline – Travail (Kifaransa)
"Umoja– Nidhamu – Kazi"
Wimbo wa taifa: L'Abidjanaise
"Wimbo wa Abidjan"
Mahali pa Kodivaa
Ramani ya Kodivaa
Mji mkuuYamoussoukro
6°51′ N 5°18′ W
Mji mkubwaAbidjan
5°20′ N 4°1′ W
Lugha rasmiKifaransa
SerikaliJamhuri
 • Rais
Alassane Ouattara
Patrick Achi
Historia
 • Kuasisi kwa jamhuri
4 Desemba 1958
 • Uhuru kutoka Ufaransa
7 Agosti 1960
Eneo
 • Jumlakm2 322 463 (ya 67)
 • Maji (asilimia)1.4
Idadi ya watu
 • Kadirio la 202329 344 847
 • Sensa ya 201422 671 331
 • Msongamano91.1/km2
SarafuFaranga ya CFA
Majira ya saaUTC+0 (GMT)
Msimbo wa simu+225
Jina la kikoa.ci
Abidjan ni mji mkubwa na muhimu zaidi kiuchumi wa Ivory Coast .

Historia

hariri

Baada ya uhuru (7 Agosti 1960) iliwahi kuwa kati ya nchi tajiri zaidi za Afrika lakini tangu mwaka 2002 uchumi na hali ya maisha kwa jumla vimeharibika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe (2002-2011).

Wakazi walikadiriwa kuwa 29,344,847 mwaka 2023, lakini sensa ya mwaka huo ilihesabu idadi ndogo zaidi: 29,389,150.

Kabila kubwa ni lile la Waakan (38%). Asilimia 22% ni wahamiaji, hasa kutoka nchi jirani (Liberia, Burkina Faso na Guinea). Asilimia 4 wana asili tofauti, hasa Ufaransa, Lebanoni, Vietnam na Hispania.

Lugha zinazotumika kawaida ni 68, lakini lugha rasmi ni Kifaransa.

Upande wa dini, Uislamu una 42.5%, Ukristo 39.8% (Kanisa Katoliki peke yake 24.9%), dini asilia za Kiafrika 2.2% na dini nyingine 0.5%. Wasio na dini ni 12.6%

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Tamka: kot divwar. Jina la Kifaransa lina maana ya "pwani ya pembe za ndovu"

Marejeo

hariri
  1. TUKI. Kamusi ya Kiswahili Sanifu (tol. la 4). uk. 784.

Viungo vya nje

hariri

Serikali

Habari

Overviews

Biashara

Orodha

Utalii

Mengineyo


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kodivaa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.