Hoda Ali ni muuguzi na mwanaharakati wa haki za binadamu anayetetea haki za wasichana kwa kufanya kampeni ya kumaliza ukeketaji wa wanawake nchini Uingereza.

Hoda Ali

Anafanya kazi kama Meneja Mradi katika Shule ya Msingi ya Perivale, moja ya shule za kwanza katika harakati za kuanzisha mpango wa kutokomeza Ukeketaji (FGM), vitendo ambavyo hufanyiwa wasichana wadogo na wa kawaida, ambapo anaamini elimu ni muhimu sana kwa kuzuia ukeketaji.

Historia ya Maisha na kazi hariri

Hoda Ali alifanyiwa ukeketaji nchini Somalia akiwa na umri wa miaka 7[1]. Alipata matatizo wakati huo ikiwemo kulazwa hospitalini kwa papo hapo, kukosa uwezo wa kupata watoto na kumaliza hedhi mapema.Hivyo sasa ameamua kufanya kampeni dhidi ya ukeketaji wa wanawake ikiwa ni pamoja na ile inayofanywa na wataalamu wa matibabu.[2][3][4]. Mnamo mwaka 2014 alianzisha kikundi cha kukuza ufahamu dhidi ya ukeketaji, ambapo tukio la kwanza lilifadhiliwa. Kampeni hii ilishinda Tuzo ya CLIO ya Mtangazaji wa Mwaka mnamo 2015, na Ali alikabidhiwa New York kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya wakala wa matangazo Ogilvy Mather.[5][6][7]. Lakini pia mnamo Machi 2018 aliteuliwa kama mtetezi wa Haki za Binadamu shirika la Amnesty International..[8][9].

Kwa sasa ni mdhamini wa shirika lililosajiliwa 28TooMany lililoanzishwa kufanya tafiti na kutoa maarifa na zana kwa wale wanaofanya kampeni kukomesha ukeketaji katika nchi za Afrika.[10].

Ushiriki hariri

Mnamo 2013 Ali alionekana kwenye waraka wa kituo cha runinga cha Channel 4 kipengele cha (The Cruel Cut), ulioteuliwa na BAFTA juu ya ukeketaji uliowasilishwa na mtaalamu wa saikolojia na mwanaharakati Leyla Hussein.[11][12]

Marejeo hariri

  1. "'FGM is child abuse. Full stop.' - Ealing News Extra". ealingnewsextra.co.uk (kwa en-GB). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-07-21. Iliwekwa mnamo 2018-05-27.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  2. "Meet the British survivors of genital mutilation", Metro, 2016-11-04. (en-GB) 
  3. Carson, Mary; Daly, Claire (2016-06-16). "The sickening trend of medicalised FGM". the Guardian (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-05-20. 
  4. Attias, Aviva. "RCM launches powerful animations to help end FGM | Royal College of Midwives". www.rcm.org.uk (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-05-27. 
  5. Commons, Jess. "Meet The Vavengers: Get To Know The Activists Working To End FGM", Refinery29. (en-GB) 
  6. "Ogilvy & Mather London Wins Grand CLIO", O&M UK. Retrieved on 2021-07-19. (en) Archived from the original on 2020-09-26. 
  7. "Mission partner's charity wins prestigious advertising award", Church Mission Society, 2015-10-01. (en) 
  8. "The Suffragette Spirit Map". Amnesty International. 2018. 
  9. Patel, Salina. "Meet the inspirational west London women defending human rights who are being celebrated in the suffragette movement", Get West London, 8 March 2018. 
  10. "About Us - 28 Too Many". www.28toomany.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-05-27. 
  11. "Bafta TV awards 2014: Winners in full", BBC News, 2014-05-18. (en-GB) 
  12. "Raising awareness about female genital mutilation: What can we do to help? - Institute of Global Health Innovation", Institute of Global Health Innovation, Imperial College London, 2014-10-27. (en-GB)